*ZIARA YA KAMATI YA UONGOZI NA FEDHA MANISPAA YA UBUNGO YAWAPA KIBARUA KIZITO WAFANYABIASHARA NA MAKAMPUNI YASIYOLIPA KODI.*
Jana uAlhamisi, Manispaa ya Ubungo iliendelea na ziara yake iliyoanza jana ya kukagua na kukusanya mapato, katika ziara hiyo ikiongozwa na Mstahiki Meya-UBUNGO, Mhe. Boniface Jacob, iliendelea na ukaguzi kwa Makampuni mbalimbali yaliyomo katika *Jengo la Ubungo Business Park,* lililopo Ubungo, jijini Dar es salaam.
Katika ziara hiyo, Manispaa ya Ubungo imebaini kuwa kuna baadhi ya Makampuni yasiyolipa kodi na yapo Makampuni yanayolipa kodi ndogo tofauti na shughuli wanazoziendesha na kukosa baadhi ya leseni za kuendeshea biashara, leseni za maghala (Godowns) na leseni za ushuru wa huduma yaani Service Levy.
Aidha, kwa wamiliki wa makampuni ambayo yalishindwa kutoa ushirikiano kwa Manispaa na kujificha, Mstahiki Meya amewatahadharisha kuwa hatua za kisheria zitachukuliwa kwa wale wanaokwepa kodi hivyo kujificha sio dawa kwani suala la ukaguzi wa leseni na shuru mbalimbali na ukusanyaji wa mapato kwa Manispaa ya Ubungo ni endelevu hivyo ni wajibu kulipa kodi na wafuate sheria.
Wakati huo huo, Mkurugenzi wa Manispaa ya UBUNGO, Ndg. Beatrice Rest Dominic alitilia mkazo suala la kuhakikisha wafanyabiashara kuwa na leseni zote muhimu kwa shughuli wanazozifanya mfano leseni za biashara, leseni za maghala, leseni za ushuru wa huduma.
Aidha, Mkurugenzi wa Manispaa aliwataka ambao wamebainika kuwa hawajalipia leseni zao kulipa mara moja kabla hawajachukuliwa hatua za kisheria kwani kwa kutokulipa kodi ni sawa na kudhulumu pato la Taifa.
Ziara hii *itaendelea* tena siku ya kesho Ijumaa katika sehemu tofauti tofauti ili kuzidi kukusanya mapato ambayo ni muhimu kwa shughuli za maendeleo ya wana ubungo na nchi nzima kwa ujumla.
*Imetolewa na Kitengo cha Habari na Uhusiano, Halmashauri ya Manispaa ya UBUNGO.*
Kibamba Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa