TANGAZO
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo anawatangazia wanachi wote kuwa tarehe 1/4/2019 siku ya jumatatu ni siku ya Upandaji miti Kitaifa. Maadhimisho hayo kimkoa yatafanyika Wilaya ya Ubungo, katika viwanja vya shule ya sekondari Kimara Kuanzia saa 2:00 asubuhi.
Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo atakuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul Makonda. Maadhimisho hayo yataambatana na shughuli za upandaji miti katika eneo la shule ya sekondari Kimara
Kauli mbiu ya mwaka huu ni “Tanzania ya Kijani inawezekana panda miti kwa maendeleo ya Viwanda”
Wananchi wote wa Wilaya ya Ubungo mnakaribishwa kushiriki katika kuadhimisha siku ya upandaji miti, kwa kupanda miti halmashauri itafikia lengo la kudhibiti mmomonyoko wa udongo, kukinga upepo mkali, kupunguza kasi ya mafuriko, kurejesha uoto uliopotea, kupendezesha mji na kuunga mkono juhudi za kitaifa na kimataifa za kukabiliana na mabadliliko ya Tabia ya nchi.
Wananchi wote mnakaribishwa.
Imetolewa na:
ROSE MPELETA
KAIMU MKURUGENZI WA MANISPAA
HALMASHAURI YA MANISPAA YA UBUNGO
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa