HALMASHAURI YA MANISPAA YA UBUNGO
TANGAZO
MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA MANISPAA YA UBUNGO NDG JOHN LIPESI KAYOMBO ANAWATANGAZIA WAFANYABIASHARA NA WANANCHI WOTE KUWA WANAPASWA KULIPA USHURU WA HUDUMA ‘ SERVICE LEVY ’AMBAO NI 0.3% YA MAUZO.
TANGAZO HILI LINAWAHUSU WAFANYABIASHARA WOTE WAKIWEMO WAMILIKI WA NYUMBA ZA KUPANGISHA NA MADUKA YA BIASHARA YANAYOTAMBULIKA KWA MAJINA BINAFSI
MALIPO HAYO YANATOZWA KWA MJIBU WA SHERIA YA FEDHA SERIKALI ZA MITAA YA MWAKA 1982 SURA YA 290 NA MAREKEBISHO YA SHERIA YA MWAKA 2012 NA SHERIA NDOGO ZA HALMASHAURI YA MWAKA 2015 IKIWA BIASHARA HAINA HESABU RASMI UTAPASWA KULIPIA VIWANGO MLINGANO (FLAT RATE) VILIVYOPANGWA .
TAFADHALI HAKIKISHA UNALIPIA USHURU HUU MARA MOJA . HATUA KALI ZA KISHERIA ZITACHUKULIWA KWA WATAKAOKAIDI AGIZO HILI.
LIMETOLEWA NA:
JOHN L. KAYOMBO
MKURUGENZI WA MANISPAA
HALMASHAURI YA MANISPAA YA UBUNGO
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa