TANGAZO
HALMASHAURI YA MANISPAA YA UBUNGO
Tangazo kwa wafugaji wote wa mifugo wanaofugia katika Manispaa ya Ubungo
Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo inawatangazia wafugaji wote wa ng’ombe, mbuzi, kondoo, nguruwe, mbwa na paka kuwa kwa mujibu wa Sheria ndogo ndogo za Halmashauri ya Jiji ya mwaka 1989 kifungu cha 80 ya Ufugaji Mifugo Mijini inayosema kuwa:-
1. Kosa kufuga mifugo mjini bila kuwa na kibali cha ufugaji,
2. Kosa kuachia mifugo kuzurura ovyo mitaani au kufungia mifugo maeneo ya barabarani,
3. Kosa kufuga mifugo bila kuwapatia chanjo dhidi ya magonjwa kwa mujibu wa maelekezo ya wataalamu wa mifugo,
4. Kosa kuwanyima haki mifugo inayofugwa, (kuwachapa mifugo, kuwanyima chakula nk),
5. Kosa kusababisha migogoro inayotokana na mfugaji kutozingatia taratibu za ufugaji hivyo kabla ya kufuga mfugaji anapaswa kupata maelekezo kutoka kwa wataalamu wa mifugo walioko kwenye Kata husika.
Hivyo wafugaji wote wanatakiwa kutoa taarifa kwa wataalamu wa mifugo walioko kwenye Kata husika kwa ajili ya kupata maelekezo Zaidi.
Manispaa ya Ubungo itafanya operesheni ya kuikamata mifugo yote inayozurura na hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa wafugaji ambao mifugo yao itakamatwa kinyume na agizo hili ikiwa ni pamoja na kufikishwa mahakamani.
Tangazo hili linatolewa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo
John L. Kayombo
Mkurugenzi
Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa