HALMASHAURI YA MANISPAA YA UBUNGO
TANGAZO
MKURUGENZI WA MANISPAA YA UBUNGO NDUGU JOHN LIPESI KAYOMBO ANAWATANGAZIA WAFANYABIASHARA WOTE WA MANISPAA YA UBUNGO , KUWA MAAFISA BIASHARA PAMOJA NA WAHASIBU WATAKUWEPO KATIKA OFISI ZA KATA YA SINZA ,MANZESE, UBUNGO NA MABIBO KUANZIA TAREHE 09/05/2017 HIVYO NDUGU MFANYABIASHARA AMBAYE UNAFANYA BIASHARA BILA LESENI AU HUJALIPIA USHURU WA HUDUMA (SERVICE LEVY), VILEO , MABANGO NA HOTEL LEVY.
HUDUMA IMESOGEZWA KARIBU HIVYO NENDA KALIPE KATIKA OFISI ZA KATA YA SINZA ,MANZESE, UBUNGO, NA MABIBO HARAKA, HADI TAREHE 12/05/2017 UNATAKIWA UWE UMELIPA BAADA YA TAREHE HIYO KUPITA UKAGUZI UTAFANYIKA NA ATAKAE BAINIKA KUTOLIPA HATUA KALI ZITACHUKULIWA KWA MUJIBU WA SHERIA KANUNI NA TARATIBU.
LIPA KODI KWA MAENDELEO YA MANISPAA YAKO
IMETOLEWA NA:
Jonh Lipesi Kayombo
MKURUGENZI WA MANISPAA
HALMASHAURI YA MANISPAA YA UBUNGO
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa