TANGAZO
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo anapenda kuwatangazia wanachi wote kuwepo kwa ugonjwa wa Homa ya Dengue kwa kuzingatia Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Afya dalili mojawapo ya Homa ya Dengue ni Homa kali ya ghafla inayodhoofisha na kuambatana na maumivu, maumivu makali ya kichwa, macho kuuma,maumivu ya viungo, kichefuchefu, kutapika,vipele ambavyo hutokea siku ya nne baada ya homa kuanza, kutokwa damu puani kwenye fizi na kuchubuka kirahisi, kwa sasa hakuna kinga ya homa ya Dengue.
Njia pekee ya kuepuka homa ya Dengue ni Kuzuia kuumwa na mbu anayesmbaza homa ya Dengue, Kufanya usafi wa Mazingira, Kuondoa mazalia ya Mbu, na kupulizia viuadudu vya kuua mbu wapevu
Mara nyingi dalili huwa sio kali na wengi hudhani ni homa ya mafua au maambukizi mengine ya Virusi, dalili hizi huanza kutokea baada ya wiki mbili lakini kwa wengi huchukua wiki moja ya kwanza na tayari utaanza kuona dalili za Dengue.
Ukiona dalili hizo au baadhi tafadhali fika kituo cha kutolea huduma ya Afya kwa uchunguzi Zaidi.
Imetolewa na:
KITENGO CHA HABARI NA UHUSIANO
HALMASHAURI YA MANISPAA YA UBUNGO
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa