HALMASHAURI YA MANISPAA YA UBUNGO
TANGAZO
MKURUGENZI WA MANISPAA YA UBUNGO ANAWATANGAZIA WAFANYABIASHARA WOTE AMBAO LESENI ZAO ZIMEISHA TAREHE 30/06/2017 WANATAKIWA WAFIKE KUHUISHA LESENI ZAO (RENEW) KUANZIA TAREHE 01/07/2017 HADI TAREHE 21/07/ 2017 BILA KULIPA KWA PENATI, BAADA YA TAREHE HIYO UTALIPIA NA PENATI KUANZIA 25% NA KILA MWEZI INAONGEZEKA 2%.
HIVYO WAFANYABIASHARA WOTE MNAHIMIZWA KUJA KULIPA KWA WAKATI ILI KUEPUKA USUMBUFU UTAKAO JITOKEZA WAKATI ZOEZI LA UKAGUZI LINALOENDELEA , PIA WAFANYABIASHARA WOTE AMBAO WANAFANYA BIASHARA ZAO BILA KUWA NA LESENI ZA BIASHARA MNAHIMIZWA KUJA KULIPIA.
MALIPO YOTE YANAFANYIKA HALMASHAURI YA MANISPAA YA UBUNGO ILIYOPO KIBAMBA DARAJANI NA KITUO CHA DALADALA SIM 2000 MAWASILIANO SINZA.
LIPA KODI KWA MAENDELEO YA MANISPAA YAKO.
IMETOLEWA NA:
JOHN LIPESI KAYOMBO
MKURUGENZI WA MANISPAA
HALMASHAURI YA MANISPAA YA UBUNGO
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa