TANGAZO KWA UMMA
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo kupitia idara ya Afya anawatangazia wananchi wote wa Manispaa ya Ubungo kuwa kutakuwa na zoezi la uchangiaji damu litakalofanyika Alhamisi ya tarehe 14/06/2018 ambayo ni siku ya uchangiaji damu duniani. Zoezi hilo litafanyika katika Hospitali ya Sinza kuanzia saa mbili kamili asubuhi hadi saa kumi na mbili kamili jioni.
Kauli mbiu ya Mwaka huu “jitoe kwa ajili ya wengine kuchangia damu”.
Wote mnakaribishwa kuchangia damu ili kusaidia jamii yetu.
Imetolewa na :
Mkurugenzi wa Manispaa
Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa