Ufugaji ni moja ya shughuli ya kiuchumi inayofanyika katika Manispaa ya Ubungo,Ufugaji ni aina ya ujasiliamali unaoruhusu mtu anayefuga mojawpo ya mifugo au zaidi ya aina moja. Mfugaji anaweza kufuga ng`ombe ,mbuzi ,kuku ,nguruwe, sungura, nyuki,samaki nk
KIPATO.
Ujasiliamali wa mifugo humwingizia mfugaji kipato na lishe kwa familia kutokana na aina ya mifugo aliyofuga,mfugaji wa kuku hupata mayai, nyama, na mbolea na mfugaji wa ,sungura na nguruwe hupata nyama na maziwa kwa mfugaji wa ng`ombe na mbuzi.
Sehemu ndogo ya mazao hayo hutumika nyumbani na kiasi kikubwa hutumika hupelekwa sokoni kwa ajili ya kujipatia kipato cha fedha na kipato hicho hutumika kwa matumizi mbalimbali ya kifamilia ikiwemo chakula, mavazi, matibabu,ada za shule, na masuala ya kijamii kama vile harusi misiba nk
Pia mbolea inayopatikana hutumika kwenye bustani za nyumbani na wafugaji wengine huuza na kupata fedha.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa