Tarehe 21/8/2020 Tamasha la Vodacom InterSchool Competition limefanyika kwa Kata ya Mbezi likihusisha shule za sekondari zilizopo katika Kata hiyo na Mgeni rasmi katika bonanza hilo ni Katibu wa Siasa na uwenezi wa CCM Mkoa Ndg.Simoni Mwakifamba ambaye alipokelewa na mwakilishi wa Afisa elimu Manispaa ya Ubungo Shima Banele.
Lengo la kufanyika kwa tamasha hilo ni kukuza vipaji vya wanafunzi,kuongeza ufanisi, kuwakuza kiafya na kuongeza umoja.
Mashindano hayo yalihusisha mpira wa miguu wa wavulana, mpira wa miguu kwa wasichana na mpira wa pete wa wasichana.
Mshindi katika mashindano hayo ilikuwa ni shule sekondari Mbezi Inn kwa upande wa mpira wa miguu na walitunukiwa medani, mpira na tisheti kutoka Vodacom pia Shule ya sekondari Mpigi Magoe iliibuka mshindi wa pili katika mashindano hayo.
"Nimefurahi kupata fursa hii kuja kujionea mashindano haya na niwapongeze waalimu na maafisa elimu kwa juhudi walizofanya na kuonyesha utofauti" Alisema hayo Mwakifamba
Aidha aliongeza kwa kusema kuwa Mazoezi ni afya na yanamfanya mwanafunzi kuimalika kiakili nani chakula cha ubongo pia.
"Elimu sio tu ya darasani tu hata michezo ni elimu pia" ilikuwa ni kauli ya Shima Banele wakati akielezea namna ambavyo mazoezi hayo yanaumuhimu kwa wanafunzi.
Mwisho aliwapongeze wanafunzi wote kwa kujitoa kwao kushiriki mazoezi hadi kufikia hatua ya kucheza mashindano hayo kwani ni hatua kubwa yenye kuibua vipaji na kuonyesha picha nzuri kwa wanafunzi hao.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa