Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mheshimiwa Kheri James Mapema tarehe 16,novemba 2021 aliongea na waandishi wa habari na kusisitiza yafuatayo
SWALA LA ULINZI NA USALAMA
•Wamiliki wa silaha wasiokuwa na kibali wanatakiwa kuzisalimisha Mapema katika Kituo chochote Cha polisi kilichokuwa karibu na asiyefanya hivyo atawajibika kwa mujibu wa sheria kwani nikosa kumiliki silaha kinyume Cha Sheria
•Aliendelea kusema kuwa Kumekua na ongezeko la matukio ya ubakaji na ulawiti kwa wanafunzi. Jambo ambalo linaendelea kwa wale wote watakaokutwa na hatia hatua zinachukuliwa na amewataka wazazi kuacha tabia ya kumaliza mambo hayo kifamilia.
•Pia ameongelea kuhusu barabara ya morogoro road kumekuwa na ajali za mara kwa mara hivyo ameendelea kuwasisitiza wafanyabiashara wote wanaofanya biashara katika maeneo ya barabara kuondoka ilikuweza kuondokana na ajali hizo.
USAFI
•Kheri amesema kutokana na Wilaya ya Ubungo kuwa ni lango la kuingilia Dar es Salaam amewataka wananchi kushiriki vyema katika program za usafi na hasa kufanya shughuli na biashara zao kwenye maeneo rasmi ili kuimarisha usafi.
•Na amewataka maafisa afya kutoa ushirikiano wa kutosha kwa viongozi wa mitaa katika kuhakikisha maeneo yote yanakuwa masafi.
•Kheri amesisitiza maeneoo yote ambayo yalikuwa yakifanyiwa Biashara na kwa sasa maeneo hayo yamekuwa wazi yaweze kufanyiwa usafi.
MIRADI YA MAENDELEO
•Kheri amemshukuru Mhe.rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutoa fedha shilingi bilioni 3.44 kwaajili ya Ujenzi wa madarasa 151 na kununua mashine ya mionzi kwa ajili ya Hospitali ya Wilaya ya Ubungo iliyopo Kimara Baruti
•Kheri Aliendelea kwa kusema kuwa Manispaa ya Ubungo inaendelea na Ujenzi huo wa madarasa ili ifikapo mwaka 2022 wanafunzi wote wa kidato cha kwanza wakapokelewe na kuanza masomo kwa pamoja
AFYA
•Aidha kheri amesema kuwa Manispaa ya Ubungo imeanzisha kampeni ya mazoezi na amesisitiza wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki katika mazoezi hayo kwaajilli ya kupambana na magonjwa yasiyoambukiza.
•Pia amewapongeza wataalam wa Idara ya afya kwa kujitoa kwao katika swala la utoaji wa chanjo ya UVIKO 19 na kuwasisitiza wananchi kuendelea kujitokeza kuchanja na kwa atakae kuwa tayari kwa hiari yake kupata chanjo hiyo basi awasiliane na yeye au Mganga Mkuu wa Manispaa ya Ubungo ile waweze kufuatwa walipo kwa ajili ya kupata chanjo hiyo.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa