Pongezi
iwapongeze wananchi wa kata ya Saranga na Ubungo Kwa ujumla kwa kazi nzuri katika kusimamia shughuli za maendeleo.
Ulinzi na Usalama
Suala la Ulinzi na Usalama linahitaji ushirikiano Kati ya wananchi na Serikali ili Ubungo yetu iwe salama, nawapongeza wenyeviti wa mitaa kwa kuunda vikundi vya ulinzi shirikishi kwa ajili ya kuimarisha ulinzi kwenye Mitaa yenu.
Ili kuhakikisha Ulinzi na Usalama unaimarika kwenye Mitaa yetu ni vema kila mmoja mwenye uwezo wa kufanya kazi awe na shughuli ya kufanya na Serikali tutahakikisha tutatengeneza mazingira bora ya kumwezesha kila mtu kufanya kazi badala ya kujihusisha na uhalifu.
Usafi
Kuna magonjwa mengi yanasababishwa na uchafu, Napenda Ubungo iwe mfano Kwa kuwa na barabara na maeneo ya wazi Safi, kila mtu afanye usafi kwenye eneo lake, niwasisitize watendaji kuzingatia usafi na tuache tabia ya kutupa taka ovyo, pandeni miti ili kuweka Wilaya yetu Safi ukizingatia Wilaya yetu ndio lango la jiji
Miradi ya maendeleo
Serikali inaleta fedha nyingi za miradi ni wajibu wenu wananchi kuilinda na kuitunza, vilevile jengeni utamaduni wa kutembelea miradi inayotekelezwa kwenye maeneo yenu ili kuifahamu lakini pia kutoa taarifa kama kuna changamoto yoyote mapema.
Kuhusu Elimu
Napenda kuwaeleza kuwa serikali inatoa Elimu bila malipo kama wazazi mtaamua kuchangia fedha ili watoto wasome masaa ya ziada hayo ni makubaliano yenu na kwa wanafunzi watakaoshingwa kuchangia wasilazimishwe hiyo ni ziada sio lazima
Chanjo ya UVIKO 19
Kuna uvumi ulioenea kuwa chanjo inapelekwa kwenye shule na inazua taharuki kwa wanafunzi wakiona gari kwenye mazingira ya shule, napenda kutoa maelezo kuwa hicho kitu hakipo na hakiwezi kutokea kwani chanjo ni hiari ya mtu. Aidha katika Wilaya yetu tunatarajia kwa na siku mbili za kutoa chanjo eneo la wazi ili wale wanaotaka kuchanja na wanakosa muda wapate huduma hiyo.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa