Waziri wa Maji Jumaa Aweso ametoa siku 14 kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Maji safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja kufikisha huduma ya maji kwa wananchi wa mtaa wa golani kata ya kimara baada ya kukosa huduma hiyo kwa muda mrefu.
Agizo hilo ametoa leo tarehe 24 desemba,2020 alipotembelea na kukagua mradi mpya wa maji unaotekelezwa katika mtaa wa Golani kata Kimara jimbo la Ubungo na kueleza kuwa huduma ya maji ni ya msingi na haina mbadala hivyo naiagiza DAWASA kukamilisha mradi huu ndani ya siku 14 ili wananchi wa golani wapate maji.
Waziri wa Maji Jumaa Aweso akizindua uchimbaji wa mtaro kwa ajili ya kutandika mabomba ya maji kwenye mradi mpya wa maji Golani kata ya kimara leo alipotembelea kata hiyo.
Katika Ziara hiyo, waziri wa maji aliongizana na Waziri wa Uwekezaji Prof. Kitila Mkumbo ambaye ni mbunge wa jimbo la Ubungo , mbunge wa kibamba Issa Mtemvu na viongozi mbalimbali wa wilaya ya ubungo.
Aweso ameeleza kuwa "Pamoja na kazi kubwa mnayoifanya DAWASA ya kusambaza maji katika jiji la Dar Es Salaam lakini maeneo ya pembezoni kama golani mnayasahau , nawakumbusha kuwa kila mtanzania ana haki ya kupata huduma ya maji safi na salama na ndio ahadi ya serikali "
Aidha waziri Aweso amewataka watendaji wa DAWASA kufainyia kazi malalamiko ya wateja wao kwa haraka kwani kwa kufanya hivyo wananchi watafurahia huduma zenu badala ya kuzipuuzia au kuzichukulia kimazoea "Wananchi wanahitaji huduma ya maji na bila maji wananchi wanatumia muda na gharama kubwa kupata maji chapeni kazi"
Aidha mhe. Waziri amewataka wananchi wa golani kuwajibika kulipa bili za maji , kulinda na kutunza miundombinu ya maji pindi mradi huo utakapokamilika ili mradi uwe endelevu.
Wananchi wa Golani wakimsikiliza kwa makini Waziri wa maji Jumaa Aweso (hayupo pichani) wakati alipotembelea mtaa huo kutatua kero ya maji iliyodumu kwa muda mrefu.
Nae Mbunge wa Jimbo la ubungo Prf. Kitila Mkumbo ambaye pia ni Waziri wa Uwekezaji amewahakikishia wananchi wa Jimbo hilo kuwa serikali itaendelea kutatua kero za wananchi ikiwemo changamoto ya barabara za pembezoni ili ziweze kupitika vizuri tofauti na hali ya sasa.
Mbunge wa Jimbo la ubungo mhe Prof Kitila Mkumbo ambaye pia ni waziri wa Uwekezaji akishiriki uchimbaji wa mtaro kwa ajili ya kuweka mabomba ya maji ili kupeleka huduma ya maji Golani.
Kwa upande wake Afisa mtendaji mkuu wa DAWASA mhandisi Cyprian Luhemeja amesema kuwa kazi ya kulanza bomba la maji lenye urefu wa kilomita 3.7 kwa mradi wa golani imeanza na ndani ya Siku 14 wananchi watapata maji kama alivyoelekeza Mhe. Waziri.
Mhandisi Luhemeja amefafanua kuwa, Kutokana na jografia ya golani kuwa na milima na mabonde mengi, huduma ya kuunganisha maji majumbani haitakuwepo badala yake yatapatikana kwenye viosi pekee.
Aidha mhandisi luhemeja amesema changamoto ya maji kwa maeneo ya pembezoni imeanza kufanyiwa kazi ampapo DAWASA inaendelea kutekeleza miradi mbalimbali yenye zaidi ya bilioni 100. Patikanaji wa maji kwa Wilaya ya ubungo upo kwa asilimia 45
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa