Hayo yamesemwa leo tarehe 14 May 2022 na Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Innocent Bashungwa alipofanya ziara katika Wilaya ya Ubungo na kutembelea barabara hiyo
ambayo imekua kero kubwa kwa wananchi wa eneo hilo.
Mhe. Bashungwa baada ya ukaguzi wa barabara hiyo ametoa maelekezo ya serikali kwa Manispaa ya Ubungo na TARURA kufanya tathmini ya gharama ya ujenzi wa barabara hiyo na kuwasilisha makadirio hayo Ofisi ya Rais TAMISEMI ndani ya siku thelathini ili serikali itoe fedha za kujenga barabara hiyo kwa kiwango cha lami.
"Kila eneo au mtaa una haki ya kujengewa barabara ya kiwango cha lami na sio maeneo ya mijini pekee , ndio maana Serikali ya awamu ya sita imesikia na imeamua kujenga barabara ya suka golani kwa kiwango cha lami ili wananchi wafurahie miundombinu bora ya barabara" alieleza Mhe. Bashungwa
Nae mbunge wa jimbo la Ubungo Mhe. Kitila Mkumbo amemshukuru Mhe. Bashungwa kwa kufika na kutoa maelekezo ya serikali ya kujenga barabara hiyo kwa kiwango cha lami.
#UbungoYetuFahariYetu
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa