Mkuu wa wilaya ya Ubungo ambaye pia ni Mwenyekiti wa baraza la biashara la Wilaya hiyo Mhe. Kisare Makori leo februari 15, 2021 amezindua baraza hilo lililojumuisha wajumbe kutoka sekta za umma na sekta binafsi ikiwa ni chombo cha kisheria cha kusimamia masuala ya biashara zao wilayani hilo.
Akizungumza kwenye kikao cha uzinduzi wa baraza hilo mwenyekiti huyo alieleza kuwa ukuaji wa uchumi unategemea zaidi biashara zinazoendeshwa na sekta binafsi kwa kulipa kodi, kutoa ajira na masuala mbalimbali ya ustawi wa jamii na Taifa kwa ujumla hivyo baraza hilo litasaidia kutengeneza mazingira bora ya kibiashara ili kuleta faida kwa wafanyabiashara na serikali.
Mwenyekiti aliendelea kueleza kuwa kupitia baraza hilo wajumbe wa sekta binafsi na sekta za umma kujengeana uelewa wa mapoja kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu uendeshaji wa biashara, ikiwemo sheria na kanuni zinazosimamia biashara pamoja na kuainisha fursa zilizopo na namna ya kuzitumia kwa lengo la kukuza uchumi.
Akisoma taarifa fupi kuhusu baraza la biashara mwakilishi kutoka baraza la biashara la Taifa (TNBC) Willy Magehema ameeleza kuwa uanzishwaji wa baraza hilo ni wa kisheria kupita waraka wa Rais Na.1 wa mwaka 2001 likiwa na lengo la kuunda jukwaa la majadiliano kati ya Sekta za Umma na Binafsi ili kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji.
Wajumbe wa baraza la biashara la wilaya ya Ubungo wakifuatilia mjadala
"Baraza hili ni chombo halali cha kisheria cha kuchambua changamoto zinazokwamisha biashara katika wilaya yenu na kuzijadili kwa pamoja na hatimaye kujenga uelewa wa pamoja kuhusu uendeshaji wa biashara unaoleta manufaa kwa pande zote mbili katika harakati za kukuza uchumi" alifafanua Magehema.
Magehema amesisitiza kuwa ameeleza baraza lina wajibu mkubwa wa kutengeneza mazingira bora ya kufanya biashara na kuwekeza, kuibua fursa za uwekezaji na kuzindua fursa hizo kupitia makongamano ya uwekezaji pamoja na kuandaa midahalo mahususi.
Aidha Magehema, alitumia nafasi hiyo kutoa rai kwa wajumbe wa baraza hilo kubuni , kushauri na kuboresha mazingira ya kibiashara ili kukaribisha wawekezaji katika maeneo ya wilaya ya Ubungo.
Kwa upande wake mwenyekiti wa wafanyabiashara sekta binafsi (TCCIA) Clement Bocco amesema kuwa kuzinduliwa kwa baraza hilo ni fursa nzuri kwa wafanyabiashara kwani litatumika kutuunganisha na sekta za umma na hatimaye kuzungumza lugha moja katika kuhakikisha wafanyabiashara anakuwa na mazingira bora kufanyia biashara na serikali kukusanya Lodi bila malalamiko.
Bocco anaamini kuwa "Ubungo ni wilaya mpya, inakua, tunategeme kwa pamoja tutahakikisha tunatumia fursa zilizopo ili kukuza biashara zenu kwa kuboresha utoaji wa huduma na kutoa /kuzalisha ajira nyingi"
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa