Baraza la madiwani Manispaa ya Ubungo lapongeza Manispaa hiyo kwa kushika nafasi ya pili katika ukusanyaji wa mapato na kufanikiwa kuvuka Lengo kwa asilimia 118 % kwa mwaka wa fedha 2021/2022
Pongezi hizo zimetolewa Leo na Mstahiki Meya Manispaa ya Ubungo Mhe. Jaffary Juma Nyaigesha na kumpongeza Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Ndugu Beatrice Dominic kwa kusimamia vyema ukusanyaji wa mapato japo Halmashauri hiyo kuwa changa.
Aidha, Aliendelea kuwataka madiwani wote kuhakikisha wanasimamia swala la ukusanyaji wa mapato ili Halmashauri iweze kufikia lengo na kusimamia vyanzo vya mapato na kubuni vyanzo vipya.
"Ni Jukumu letu sote kuhakikisha mapato yanakusanywa tukisaidiana kwa pamoja tutafikia malengo" alisisita Nyaigesha
Halikadhalika, Madiwani hao waliweza kuwasilisha Taarifa za kata zao pamoja na changamoto ambazo zinatakiwa kupatiwa kupatiwa ufumbuzi.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa