Baraza hilo limefanyika tarehe 15/11 katika Ukumbi uliopo katika ofisi za Mkuu wa Wilaya likiendeshwa na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo Mhe. Boniface Jacob ambaye pia ni Diwani wa kata ya Ubungo na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo *Bi.Beatrice Dominic*, Madiwani kutoka kata zote, wakuu wa Idara na waalikwa kutoka sehemu tofauti tofauti.
Wakati akifungua baraza hilo Mstahiki Meya alisisitiza kuzingatia kwa umakini uendeshaji wa kufata maadili katika kazi na kuzingatia misingi sahihi katika kazi na kuzungumzia changamoto chache ambazo zinaonekana zihakikishwe zinazingatiwa ipasavyo na kufanyiwa ufumbuzi.
Vilevile Mhe.Boniface aliutaka uongozi wa Manispaa kushilikiana na Madiwani katika miradi ya maendeleo hususani katika ujenzi wa hospitali ya Wilaya.
Nae Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Bi. Beatrice Dominic aliahidi kuhakikisha anaongeza mapato ya Halmashauri kwa kushirikiana na watendaji wake.
Nishukuru kwa Mhe. Rais kutoa fedha ambazo zitatumika kujenga hospitali ya Wilaya ya Ubungo na haya yote yanafanywa na rais wetu wa awamu ya tano, fedha zilizotolewa ni kwa ajili ya hospitali ya Wilaya naomba kusisitiza, aliongeza Mkurugenzi
Aidha alitolea ufafanuzi wa maswali yaliyotakiwa yapatiwe ufumbuzi kutoka kwa wajumbe na kutolea majibu kwa maswali yote yaliyokua yanahitaji kutolewa majibu yake ya papo kwa papo .
Pia baadhi ya madiwani walitoa pongezi kwa maendeleo mbayo Manispaa inayafanya na kuongelea changamoto ambazo pia zinatokea na kuomba zipatiwe ufumbuzi na Mkurugenzi na baadhi ya wataalam kuhakikisha wanasimamia ipasavyo kazi zao. Baraza hilo limefanyika leo katika Ukumbi uliopo katika ofisi za Mkuu wa Wilaya likiendeshwa na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo Mhe. Boniface Jacob ambaye pia ni Diwani wa kata ya Ubungo na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Bi.Beatrice Dominic , Madiwani kutoka kata zote, wakuu wa Idara na waalikwa kutoka sehemu tofauti tofauti.
Wakati akifungua baraza hilo Mstahiki Meya alisisitiza kuzingatia kwa umakini uendeshaji wa kufata maadili katika kazi na kuzingatia misingi sahihi katika kazi na kuzungumzia changamoto chache ambazo zinaonekana zihakikishwe zinazingatiwa ipasavyo na kufanyiwa ufumbuzi. Vilevile Mhe.Boniface aliutaka uongozi wa Manispaa kushilikiana na Madiwani katika miradi ya maendeleo hususani katika ujenzi wa hospitali ya Wilaya.
Nae Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Bi. Beatrice Dominic aliahidi kuhakikisha anaongeza mapato ya Halmashauri kwa kushirikiana na watendaji wake. Nishukuru kwa Mhe. Rais kutoa fedha ambazo zitatumika kujenga hospitali ya Wilaya ya Ubungo na haya yote yanafanywa na rais wetu wa awamu ya tano, fedha zilizotolewa ni kwa ajili ya hospitali ya Wilaya naomba kusisitiza,"* aliongeza Mkurugenzi. Aidha alitolea ufafanuzi wa maswali yaliyotakiwa yapatiwe ufumbuzi kutoka kwa wajumbe na kutolea majibu kwa maswali yote yaliyokua yanahitaji kutolewa majibu yake ya papo kwa papo . Pia baadhi ya madiwani walitoa pongezi kwa maendeleo mbayo Manispaa inayafanya na kuongelea changamoto ambazo pia zinatokea na kuomba zipatiwe ufumbuzi na Mkurugenzi na baadhi ya wataalam kuhakikisha wanasimamia ipasavyo kazi zao.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa