Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo imefanya Baraza la madiwani robo ya tatu kwa mwaka wa fedha 2019/2020 la kupokea taarifa za kata katika ukumbi wa Little Flower uliopo Mbezi.
Baraza hilo limehudhuriwa na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo Mhe.Boniphace Jacob na Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo ambaye pia ni Afisa Kilimo wa Manispaa Happiness Mbelle, Madiwani na wakuu wa Idara na Vitengo.
Katika Baraza hilo kila Diwani alipata fursa ya kuwasilisha taarifa yake ya maendeleo ya kata kwa wajumbe wa baraza hilo.
Pia katika Baraza hilo hoja kubwa iliyojitokeza ni kuhusiana na suala zima la janga zima la korona.
Wakati akitoa ufafanuzi juu ya jitihada ambazo Manispaa imefanya kuhakikisha inashirikiana na serikali kupambana na ugonjwa wa korona, Happiness alisema kuwa Manispaa imekuwa mstari wa mbele kutoa vifaa na kuhakikisha inapeleka matangazo na elimu katika masoko, stendi za mabasi na kutoa elimu kwa wananchi wa Ubungo kuhusiana na Ugonjwa wa korona na namna ya kuchukua tahadhari.
Aidha Meya alishauri suala la mikopo iliyotolewa kwa vikundi vya wajasiriamali ni muhimu pesa zikafuatiliwa kwa waliokopeshwa kuhakikisha pesa hizo zinarejeshwa ili wananchi wengine wenye sifa waweze kukopeshwa.
Mwisho Mstahiki Meya alisisitiza wajumbe na wageni kujikinga na korona kwa kuzingatia masharti na tahadhari zinazotolewa na Idara ya Afya.
Aidha aliwashukuru wajumbe na wageni wote kwa kuhudhuria mkutano huo wa baraza na kusisitiza ushirikiano katika kuendeleza maendeleo katika Manispaa ya Ubungo.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa