Baraza la Madiwani la Manispaa ya Ubungo limeazimia Mtendaji wa Kata ya Goba, Mtendaji wa Mtaa wa Kinzudi pamoja na mwenyekiti wa mtaa huo kutoa maelezo ya kina juu ya kutotoa taarifa za uvamizi wa eneo la mtaa wa Kinzudi kwenye eneo linalofahamika kama shamba la mzungu lenye ukubwa wa ekari 10
Azimio hilo limeazimiwa leo tarehe 09/02/2023 wakati wa kikao cha baraza la kawaida la Madiwani robo ya pili kwa mwaka wa fedha 2022/2023
Sambamba na azimio hilo baraza hilo limeazimia kuwa shughuli zozote za kuendeleza eneo hilo zisifanyike hadi mipaka ya eneo hilo itakapo fufuliwa.
Maazimio hayo yamefanyika kutokana na hoja iliyoibuliwa mnamo tarehe 08/02/2023 wakati wa kikao cha baraza la kupokea taarifa za utekelezaji za Kata 14 zilizopo Manispaa hiyo ambapo Diwani wa Kata ya Goba Mhe. Esther Ndoha alipowasilisha hoja ya uvamizi wa eneo hilo.
Akiongea Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Hashimu Komba ameitaka Manispaa hiyo kuhakikisha maeneo yote yanayomilikiwa na Manispaa hiyo yapimwe na kulindwa ili kuepukana na uvamizi wa maeneo hayo.
Aidha, Mhe. Komba amewataka viongozi na wataalamu wa Manispaa hiyo kuendelea kufanya kazi kwa ushirikiano, kuongeza kasi juu ya suala la urasimishaji na kusimamia maeneo ya huduma ikiwemo barabara na maji pamoja na uwajibikaji.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa hiyo amesema maazimio hayo yatatekelezwa na kufanyiwa kazi kwa wakati kwa maslahi mapana ya wananchi na amewataka watalamu wa Manispaa hiyo kuendelea kuwajibika kwa pamoja juu ya kuwahudumia wananchi.
Nae Diwani wa Kata ya Makurumla Mhe. Bakari Kimwanga amempongeza Mhe Ndoha kwa kuleta hoja ya uvamizi wa eneo hilo kwenye baraza kwa maslahi mapana ya wananchi wa Kinzudi na Goba kwa ujumla.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa