-Jumla ya maeneo 285 yalibanishwa katika kata tano tu zilizotembelewa.
-Katika maeneo hayo, Manispaa inaweza kukusanya milioni 564.4 kwa mwaka.
Baraza la Madiwani la Manispaa ya Ubungo Novemba 4, 2021 limepokea ripoti ya Kamati maalumu iliyoundwa kutembelea na kuchunguza maeneo ya wazi katika kata tano za Manispaa hiyo kama chanzo mojawapo cha Mapato kwa Manispaa.
Kamati hiyo ilitembelea na kukagua maeneo ya wazi yaliyopo katika kata za *Sinza, Manzese, Mburahati, Goba na Makurumla
Akiongea wakati wa kukabidhi ripoti hiyo, Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Eliamu Manumbu amesema kuwa, Kamati ilifanikiwa kutembelea maeneo *285 ambapo maeneo 51 ni ya wazi, 211 vizimba vya maji na maeneo mapya 23 yanayoweza kukusanya kiasi cha shilingi 564,352,960 kwa mwaka mzima kwa kata tano zilizotembelewa na kukaguliwa.
Aidha, Mwenyekiti ameendelea kueleza kuwa, Kamati imependekeza zoezi hilo lifanyike kwenye kata 9 zilizobaki ili kubaini maeneo hayo ambayo ni chanzo kikubwa cha Mapato kwa Manispaa hususani katika kipindi hiki ambacho bajeti ya Manispaa hiyo imepanda kutoka bilioni 18 Hadi kufikia bilioni 27 Kwa mwaka huu wa fedha.
Mwenyekiti wa Kamati amefafanua kuwa milioni 564.4 zilibainishwa na Kamati kukusanywa katika maeneo hayo haijajumuisha tozo za maeneo ya wazi ambayo ukubwa halisi haukupimwa.
Akiongea baada ya kupokea ripoti hiyo, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo Mhe. Jaffary Juma Nyaigesha ameipongeza kamati Kwa kazi nzuri iliyofanya na kuahidi kufanyia kazi mapendekezo ya Kamati hiyo ikiwemo kubaini maeneo ya wazi Kwa kata 9 zilibaki pamoja na kuweka mikakati ya kuanza kukusanya mapato kupitia chanzo hicho.
Aidha, kutokana na kazi nzuri iliyofanywa na Kamati hiyo , wajumbe wa Baraza hilo wameazimia kuipongeza Kamati hiyo Kwa kutoa motisha Kwa wajumbe wa Kamati hiyo huku Mtendaji wa Mtaa wa NHC kata ya Mburahati kupewa tuzo ya uzalendo na fedha tasilimu milioni moja Kwa ushirikiano mkubwa alioonesha Kwa Kamati.
Kamati hii iliyojumuisha waheshimiwa Madiwani, wataalamu, na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ni utekelezaji wa azimio la Mkutano wa Baraza la Madiwani lililoketi mwezi April mwaka huu lengo ikiwa ni kuyatambua maeneo hayo ikiwa ni moja ya chanzo cha Mapato ya Halmashauri.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa