Baraza la madiwani Manispaa ya Ubungo lasisitiza ukusanyaji wa mapato na uzingatiaji wa usimamizi wa vyanzo vilivyoainishwa kwaajili ya ukusanyaji wa mapato ili kuwezesha maendeleo ya Halmashauri
Hayo yemeelezwa Leo katika Baraza la madiwani la kuwasilisha taarifa za robo ambapo Wajumbe wa baraza hilo walisisitiza ukusanyaji wa mapato utiliwe kipaumbele kwa kuzingatia vyanzo na ubunifu wa vyanzo vingine vitakavyoongeza mapato
Aidha Mstahiki meya Manispaa ya Ubungo alisisitiza Kila mmoja kushiriki ipasavyo katika usimamizi wa vyanzo vya mapato
"Tusimamie kwa uweredi ili tuepukane na upotevu wa mapato" alieleza Nyaigesha
Swala la mapato ni letu sote , Kila mmoja anawajibu wa kuhakikisha anachangia upatikaji wa mapato kwa kuangalia vyanzo vinavyopoteza mapato viweze kusimamiwa
Aidha pongezi zimetolewa kwa Uongozi wa wilaya ya Ubungo kwa Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya Kheri James kwa usimamizi mzuri wa Ujenzi wa madarasa 151 yaliyojengwa kwa shule 21 zilizopo Manispaa ya Ubungo
Alikadhalika Mstahiki Meya ameendelea kuwataka wataalam kuhakikisha wanafata miongozo na Sheria za utumishi
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa