Baraza la madiwani Manispaa ya Ubungo mapema leo tarehe 27 Mei, 2022 lasisitiza ukusanyaji wa mapato ili kuweza kufikia Lengo.
Akiongea wakati wa Baraza Hilo Mhe. Mstahiki Meya Manispaa ya Ubungo Jaffary Juma Nyaigesha ameendelea kusisitiza ukusanyaji wa mapato kuwa kipaumbele.
Akizungumza katika Baraza hilo Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mheshimiwa Kheri James amepongeze Baraza la Madiwani kwa kuwezesha mfuko wa vijana, wanawake na watu wenye ulemavu kupata mikopo ambayo leo hii imekabidhiwa hundi ya Milioni 804 kwa wajasiriamali hao.
Aidha amesisitiza swala Watumishi kushiriki kwenye mikutano ya wananchi ili kuweza kujibu moja kwa moja changamoto mbalimbali za wananchi ili kufanya wananchi waendelee kuiamini Serikali yao.
"Ubungo iko salama na ni wapongeze Wabunge wa majimbo yetu kwa kuendelea kupambana na kero za wananchi wa Wilaya ya Ubungo na kupambana katika kuhakikisha miradi mbalimbali ya muhimu inatelezwa ubungo" alisema Kheri
Aidha watumishi wa manispaa hioyo wametakiwa kusimamia vema utekalezazi wa miradi ya maendeleo na ukusanyaji wa mapato.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa