Baraza la Madiwani la Manispaa ya Ubungo limeridhishwa na kasi ya ukusanyaji wa Mapato kwa mwaka wa fedha ulioishia Juni 30 mwaka huu Kwa kufanikiwa kukusanya asilimia 102 ya mapato ya ndani.
Madiwani wameonesha kuridhika na ukusanyaji huo wa Mapato baada ya kupokea taarifa za Utekelezaji wa shughuli mbalimbali kwa kipindi cha robo ya nne kilichoishia Juni 30,2021
Wakichangia taarifa hizo waheshimiwa Madiwani wamesema "Tunatoa pongezi kwa menejimenti Kwa usimamizi mzuri katika ukusanyaji wa mapato na kufanikiwa kuvuka lengo"
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mheshimiwa Kheri James, amewataka watumishi kuendelea kufanya kazi kwa bidii katika kutekeleza shughuli za Serikali na kuboresha huduma kwa Wananchi
Aidha DC Kheri, ametumia mkutano huo wa Baraza la Madiwani kueleza juu ya ujio wa Mwenge wa Uhuru tarehe 19.08.2021 ambapo utapokelewa kibamba CCM Darajani na utakesha Mburahati katika uwanja wa barafu
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa