Leo tarehe 04 Novemba, 2021 Wajumbe wa Baraza la Madiwani, Manispaa ya Ubungo wamepata mafunzo ya kujengewa uelewa juu ya masuala ya Maadili ya Utumishi wa Umma hususani katika ujazaji wa fomu za Mali na Madeni kwa Viongozi wa Umma.
Mafunzo hayo yametolewa na Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma ambapo wajumbe hao wameelezwa wajibu na mienendo wanayopaswa kuzigatia wakiwa kama Viongozi wa Umma.
Mgongano wa kimaslahi, matumizi mabaya ya madaraka na mienendo isiyofaa kwa Viongozi na Watumishi wa Umma yameainishwa katika mafunzo hayo kuwa ni miongoni mwa tabia na mienendo isiyofaa kwa Kiongozi wa Umma.
Kupitia mafunzo hayo, wajumbe walielezwa kuwa endapo Kiongozi wa Umma atatenda makosa ya uvunjifu wa Maadili ya Utumishi wa umma anaweza kufukuzwa kazi, kushushwa cheo, kuvuliwa madaraka, kupewa kalipio na adhabu nyinginezo.
Wajumbe wa baraza la madiwani wakiwa kwenye mafunzo ya Maadili kwa Viongozi wa Umma
Alifafanua kuhusu madhara ya migongano ya kimaslahi kwa Viongozi, mwezeshaji wa mafunzo hayo ndugu Njenga Silvanus amesema ni kuvunja misingi ya Utawala Bora kwa kutumia madaraka kwa maslai binafsi badala ya maslahi ya Umma.
Aidha, wajumbe walipitishwa namna ya ujazaji wa fomu ya kiapo ambapo kila Kiongozi wa Umma anapaswa kuijaza kwa usahihi kwa mujibu wa Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma ya Mwaka Na. 13 ya mwaka 1995 kila kiongozi anapaswa kuwa amejaza na kuwasilisha fomu hiyo kabla au ifikiapo tarehe 30 Disemba, 2021.
Aidha, Sekretarieti imesisitiza kiapo hicho kinapaswa kujazwa kwa umakini na kwa uhadilifu ili kuepuka taharuki zinazoweza kutokea pindi kiapo kitakapokuwa kimejazwa tofauti.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa