Baraza hilo limefanyika katika ukumbi wa Little Flower uliopo Mbezi na kuongozwa na Kaimu Mstahiki Meya Ramadhan Kwangaya na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Beatrice Dominic
Baraza hilo limehudhuriwa pia na Mwenyekiti wa Chama cha CCM Wilaya ya Ubungo Ndg. Lucas Mgonja ,Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe.Kisare Makori, Katibu Tawala wa Wilaya ya Ubungo Ndg.James Mkumbo,Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya, Madiwani,na Watalaam kutoka Manispaa ya Ubungo.
Lengo la Baraza hilo ni kupitia taarifa za utekelezaji wa shughuli za Halmashauri kwa kamati zote robo ya nne kuanzia April hadi Mei.
Sambamba na hilo Katibu alipata nafasi ya kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa shughuli za Halmashauri kuanzia Julai 2016 hadi Mei 2020.
Aidha Shughuli za kamati kwa kamati zote zilizoundwa kwa kipindi chote ulienda vizuri kutoka kuanzishwa kwa kamati zote mpaka siku ya leo ambayo Baraza hilo la mwisho limenyika.
Vile vile Madiwani walishukuru kwa ushirikiano ambao ulitolewa na wataalam kutoka Halmashauri kwa kuleta mabadiliko kwa Manispaa ya Ubungo.
Sambamba na hilo Mkuu wa Wilaya aliwashukuru madiwani wote kwa kipindi chote walichokuwepo katika utekelezaji wa majukumu yao, nakuwataka wale wote watakaoshiriki uchaguzi wafanye kwa amani na kuzingatia uaminifu,uadlifu na kufanya kazi kwa uweledi.
”Nitoe shukrani pia kwa mweshimiwa Rais wa awamu ya tano Dk.John Pombe Magufuli kwa maendeleo anayoyaleta katika nchi yetu". Aliongezea Mkuu wa Wilaya
Mwisho Kaimu Mstahiki Meya alimshukuru Mkurugenzi pamoja na wataalam wote wa Manispaa kwa kushirikiana na kujitoa kwenye suala la kuleta maendeleo ya Halmashauri ya Ubungo na juhudi zikaendelee kuiendeleza Manispaa Ubungo.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa