Manispaa ya Ubungo imepokea madarasa mawili yaliyojengwa CRDB na madawati 125 katika shule ya Sekondari ya Mashujaa iliyopo kata ya Sinza katika Manispaa hiyo lengo ikiwa ni kuunga mkono juhudi za Serikali katika kupunguza changamoto ya upungufu wa madasara na madawati kwenye shule.
Akikabidhi miundombinu hiyo Meneja mwandamizi wa uwekezaji Kwa jamii kwenye benki hiyo ndugu Joycelean Makule amesema kuwa ujenzi huo wa madarasa na madawati umegharimu kiasi cha Tsh Milioni 50 lengo ikiwa ni kuisaidai serikali kupitia sera yao ya msaada kwa jamii.
Meneja mwandamizi wa uwekezaji kwa jamii CRDB Joycelean amesema Kwa niaba ya Benki ya CRDB wameahidi kushirikiana bega kwa bega na serikali katika kutatua changamoto mbalimbali kupitia sera yao ya msaada kwa jamii (Coorparate Social Investiment) hivyo wameamua kuboresha miundombinu ya elimu kwa ujenzi wa madarasa na madawati hayo.
Akiongea baada ya kupokea miundombinu hiyo Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe. Kheri James ameipongezi Benki CRDB Kupitia sera yao ya msaada kwa jamii (Coorporate Social Investment) ambayo imekuwa ikisaidia kwa kiasi kikubwa katika kutatua changamoto mbalimbali zinazoikumba jamii katika maswala mbalimbali ya kijamii na kuwaomba kuendelea kushirikiana na serikali katika kutatua changamoto.
Aidha, James amewataka walimu na wanafunzi kuhakikisha wanayatumia na kuyatunza vizuri madawati na madarasa hayo ili yaweze kutumika kwa muda mrefu na kunufaisha watoto wengi waliopo sasa na watakaokuja baadae.
Pia amesisitiza kuwa shule hizo ni Mali ya Umma hivyo ni wajibu wa Umma kupitia nguvu na nyenzo tulizonazo kusaidia shule za Umma kufanya vizuri kwa maana ya miundombinu na kuimarisha ufaulu. Na amewaomba wadau wengine wajitokeze kuhakikisha ufaulu na miundombinu inaimarika mashuleni.
“Lengo la serikali si kuwa tu na shule na madawati mazuri bali ni kuwa na shule nzuri, madawati mazuri yatakayochochea ukuaji wa taaluma na ufaulu kwa wanafunzi”. Alisema James.
James amempongeza aliyekuwa Mkuu wa Shule hiyo ambae amestaafu kwa sasa kwa kupambana kwake katika kuhakikisha shule hiyo inakuwa na miundombinu bora, ameipongeza bodi ya shule kwa juhudi zao, serikali imepanga kuanzisha A level shuleni hapo.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa