Benki ya NMB imeikabidhi Manispaa ya Ubungo msaada wa vifaa vya kuboresha huduma za afya na elimu vyenye thamani ya Tsh Milioni 27.
Akikabidhi vifaa hivyo meneja wa NMB Donatus Richard alieleza kuwa vifaa hivyo vinajumuisha
vitanda vya kujifungulia 5, vitanda na magodoro ya kawaida 10,mashine za kupima presha 10 na pazia za wodini 10 kwa ajili ya hospitali ya Wilaya, viti na meza 35 kwa ajili ya walimu na viti na meza 110 kwa wanafunzi shule ya msingi Kwembe na Sekondari ya Urafiki.
Makabidhiano hayo yamefanyika leo Juni 7,2022 ambapo Ndugu Richard ameeleza kuwa benki hiyo inaendelea kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya sita na hivyo kwa kuipa kipaumbele agenda ya afya na elimu wameamua kutoa vifaa hivyo.
“Elimu na Afya ni agenda muhimu kwa benki yetu kutokana na umuhimu wake sisi kama wadau tumeona tuunge mkono juhudi za Serikali katika agenda hizi muhimu” Alisema Richard
Nae Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo Jafary Nyaigesha ameipongeza benki hiyo kwa jitihada zao za kuendelea kushirikiana na Serikali kwa kutoa misaada mbalimbali kwa jamii. Na ameipongeza Serikali ya awamu ya sita kwa kuiwezesha Manispaa kwa utekelezaji wa miradi yakimkakati hadi kupelekea Benki ya NMB kutoa vifaa hivyo na ameiahidi benki hiyo kuwa vifaa hivyo vitatunzwa kwa maslahi ya wana Ubungo.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe. Kheri James ametoa wito kwa Taasisi nyingine kuiga mfano wa walichokifanya benki ya NMB kwani faida kubwa wanazozipata ni kutokana na michango ya wanajamii. Na ameipongeza benki hiyo kwa jinsi inavyojitoa kwa Serikali yao kwa kutoa misaada mbalimbali yakuiwezesha jamii.
James ameendelea kueleza mbali na kuwa Serikali inaiwezesha jamii kwenye masuala ya elimu, afya na sekta nyinginezo lakini pia NMB imekuwa mstari wa mbele katika kuunga mkono juhudi hizo.
Kwani vitanda vilivyotelewa kwa ajili ya akina mama vitakuwa na mchango mkubwa katika kuwawezasha akina mama kuwa kwenye mazingira mazuri wakati wa uzazi lakini walimu watafanya kazi kwenye mazingira mazuri na wanafunzi watasoma kwenye mazingira mazuri. Na amewasihi Shule ya Msingi Kwembe, Sekondari ya Urafiki na Hospitali ya Wilaya kutunza vifaa hivyo ikiwa kama ni ishara ya kutoa shukrani kwa NMB.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa