Bodi ya afya Manispaa ya Ubungo imefanya ziara ya kukagua miradi ya afya inayotekelezwa katika Manispaa hiyo na kutoa pongezi za uendeshaji wa miradi kwa kuzingatia viwango ikiwemo ubora wa majengo pamoja na kasi ya uendeshaji
Akizungumza wakati wa ziara hiyo Mwenyekiti wa kamati Ndg. Allan Sempori amesisitiza muda uliopangwa wa uendeshaji wa miradi kukamilika uendelee kuzingatiwa na katika maeneo ambayo yameonekana kuna changamoto ya barabara sio rafiki kwa wagonjwa kufikia Vituo hivyo ziweze kutengenezwa kuwezesha upatikanaji wa huduma kwa wagonjwa kufikiwa kwa urahisi
Aidha, wajumbe wa kamati za Afya katika Vituo vya afya wameombwa kuzingatia thamani ya fedha zinazotumika katika Ujenzi na pia kufanya ufuatiliaji mzuri wa hatua kwa hatua toka mradi unaanza mpaka unamalizika
"Mmoja wa wajumbe hao aliwataka waganga wafawidhi katika Vituo kuwashirikisha wajumbe wa kamati za bodi za Vituo kwenye Kila hatua kuepusha kutokea kwa changamoto mwishoni"
Halikadhalika , wajumbe waliendelea kusisitiza katika changamoto zilizopatikana kwenye baadhi ya miradi kutiliwa mkazo kuhakikisha zinafanyiwa kazi ikiwa ni moja ya kazi ya kutimiza majukumu ya kamati.
Miradi iliyotembelewa na bodi hiyo ni pamoja na Mradi wa Kituo Cha Afya Amani kilichopo Kata ya kwembe, Kituo Cha Afya Goba, zahanati ya Mpigi Magoe, Hospitali ya Wilaya ya Ubungo iliyopo Baruti na Kituo Cha Afya Cha sinza palestina.
#UbungoYetuFahariYetu
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa