Hayo yalisemwa na mstahiki Meya Manispaa ya ubungo Mhe.Japhari nyaigesha wakati wa kikao hicho kilichofanyika tarehe 17/3/2021 kikiwa na lengo la kupitia taarifa ya miradi ya maendeleo ya afya kwa kipindi cha oktoba hadi disemba na ujenzi wa miradi pamoja na usimamizi shirikishi wa vituo vya afya .
Nyaigesha aliwataka Wajumbe kuhakikisha wanaendelea na kasi waliyokuwa nayo ilikuleta mandeleo kwa wananchi wa ubungo kwa kuboresha miundombinu ya afya na kusimamia ipasavyo
"Ubungo imeendelea kufanya vizuri kwenye sekta ya afya hasa katika hutoaji wa huduma na ujenzi wa vituo vya afya na mfano mzuri kituo cha afya kimara ni kwa sababu ya kujituma kwenu niwapongeze sana kamati hii" Alisema hayo Nyaigesha
Sambamba na hayo Mwenyekiti wa bodi hiyo Ndg.Israel Sostheness aliwashauri kamati kuwahusisha wadau mbalimbali na kutafuta vyanzo mbalimbali vya fedha ili kusaidia katika maswala ya afya ili kuboresha zaidi miundombinu ya afya na ustawi wa afya kwa wana ubungo
Pia kamati ilishauriwa kuweza kufanya maboresho na upanuzi wa kituo cha afya cha mbezi kutokana na eneo hilo kuwa na mkusanyiko mkubwa watu kwa sasa hivyo mahitaji kwaajili ya huduma ya afya kuongezeka kwa kasi
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa