Leo tarehe 24/06/2022 Bodi ya Afya Manispaa ya Ubungo imefanya kikao cha robo ya tatu kwa ajili ya kupitia taarifa ya utekelezaji Idara ya Afya na mapato na matumizi kwa kipindi cha januari hadi machi 2021/2022.
Katika taarifa hiyo Bodi imeweza kuona namna shughuli mbalimbali za Idara ya Afya zinavyotekelezwa kupitia vitengo vyake ikiwemo chanjo, malaria, huduma ya mama na mtoto, dawa, ustawi wa jamii, bima ya iCHF iliyoboreshwa na NHIF, HIV, Afya ya Kinga na Lishe.
Akiongea katika kikao hicho Mwenyekiti wa Bodi hiyo Bw. Allan Sempori ameipongeza Manispaa hiyo kwa namna inavyotekeleza majukum yake kwa ufanisi hasa kwa kudhibiti matumizi na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya Maendeleo kwa ufanisi.
Aidha ameipongeza Manispaa hiyoh kwa kupata hati safi mfululizo na hii nikutokana na udhibiti wa mapato na matumizi kama ambavyo wamejionea kwenye taarifa ya mapato na matumizi ya vituo vyake vya kutolea huduma za afya.
Kwa upande wake Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo Mhe. Jafar Nyaigesha ameipongeza Bodi hiyo kwa namna inavyojitoa katika kuhakikisha kuwa maslahi ya Umma yanafuatwa hasa kwenye sekta hii nyeti ya Afya na kuiomba kuendelea kuishauri Manispaa pale inapobidi ili kuendelea kuipa nguvu Idara hii katika utekelezaji wa majukum yake kwa maslahi ya wananchi.
Aidha ameitaka Bodi kuwa chachu kwa wananchi kukata bima ya iCHF iliyoboreshwa ili kuwa na uhakika wa matibabu muda wote na hivyo kuisaidia Serikali kuwa na wananchi wenye kujali afya zao.
Nae Katibu wa Bodi hiyo ambae ni Mganga Mkuu wa Manispaa hiyo Bw. Peter Nsanya ameeleza kuwa vyanzo vikuu vya mapato vya Idara ya Afya ni iCHF, NHIF, Mapato ya papo kwa papo na Fedha za Mfuko wa pamoja.
Sambamba na hayo Nsanya ameeleza maoni yote yaliyotolewa na wajumbe wa Bodi hiyo yatafanyiwa kazi kwa maslahi mapana ya wananchi.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa