Mapema Leo tarehe 24/2/2023 bodi ya Afya manispaa ya Ubungo imeweza kupitia na kujadili taarifa ya utendaji kazi kwa idara ya afya kwa robo ya pili na kuipongeza kwa utoaji mzuri wa huduma za afya katika vituo sambamba na kuwataka changamoto zilizowasilishwa na kamati ziweze kutafutiwa Suluhu
akisoma taarifa ya utekelezaji kwa robo ya pili Dk. Catherine Saguki amesema kuwa idara ya afya katika utoaji wa chanjo ya polio kwa awamu ya nne watoto 283,357 sawa na 135% walichanjwa.
Aliendelea kwa kusema kuwa, Jumla ya wakina mama 4779 walijifungua na hakukua na kifo cha mzazi kilichotokea, mashauri 86 ya ndoa yameshughulikiwa, 65 yamesuluhishwa na 14 yanaendelea kushughilikiwa
Na pia huduma ngazi ya jamii elimu imeweza kutolewa kuhusu chanjo, elimu ya kujikinga na magonjwa, uchunguzi wa awali wa magonjwa, na magonjwa mbalimbali
Idara pia imeweza kufanya uhamasishaji na kufanikiwa kukusanya damu salama chupa 755 sawa na 80.9% ambalo ni lengo kwa robo hiyo.
Aidha, Wajumbe walipendekeza bodi iweze kutembelea miradi mara kwa mara ili iweze kujua hali za miradi ilivyo
Halikadhalika, Wajumbe waliagiza watoa huduma katika vituo wafate maadili ya kazi kwa kuhakikisha wanatoa huduma kwa wananchi kwa uadilifu
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa