Kamati ya CAMFED Wilaya ya Ubungo yenye wajibu wa kusaidia watoto wa kike wanaoishi katika mazingira hatarishi, leo Machi 31, 2022 imekutana na kufanya kikao kazi kwa ajili ya kujengewa uelewa wa majukumu yake ikiwemo kuhamisha jamii kuchangia mahitaji muhimu kwa watoto wa kike wanaoishi mazingira hatarishi.
Kupitia kikao hicho kilichoongozwa na wataalamu kutoka shirika la CAMFED, kamati ina wajibu wa kusimamia mchakato wa kuwatambua watoto hao kwa kuzingatia kigezo cha kuishi katika mazingira hatarishi ili wawe wanufaika na mradi huo unaofadhiliwa na shirika CAMFED ambapo watasaidiwa mahitaji Maalumu ikiwemo vifaa vya shule, Sare na nauli ya kwenda shule na hivyo kufurahia masomo kama watoto wengine.
Kwa Wilaya ya Ubungo, Jumla ya shule 10 za Sekondari zitanufaika na mradi huo ambapo pamoja na wanafunzi hao kupata ufadhili wa mahitaji Mhimu ya shule lakini pia watapata huduma ya ushauri wa kisaikolojia na Elimu ya afya ya uzazi
Katika kufanikisha kazi hii, Kamati ya CAMFED Wilaya itasaidiwa na Kamati za shule na walimu walezi katika shule hizo ambao wanachaguliwa na wanafunzi wenyewe kutokana na kukubalika na wanafunzi na uwezo wa kusikiliza na kutatua changamoto zao kwa haraka.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa