Katika kuendeleza kampeni ya Safisha, Pendezesha Dar Es Salaam Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Bi. Beatrice Dominic amewataka wananchi kuendelea kulipa ada za taka kulingana na taratibu zilizowekwa kwenye mitaa yao kama ambavyo sheria inawataka ili kuwezesha taka kuzolewa kwenye maeneo yao.
Hayo ameyasema leo tarehe 28/05/2022 wakati wa usafi wa mwisho wa mwezi uliofanyika kata ya Mabibo barabara ya NIT ulioenda sambamba na upandaji wa miti. Viongozi mbalimbali wa chama, viongozi wa chuo cha NIT, kikundi cha scout, Miss Utalii Dar es Salaam Angela Geradi Steven, pamoja na wananchi.
Mstahiki Meya wa Manspaa ya Ubungo Mhe. Jaffary Juma Nyaigesha akipanda mti kwenye zoezi la usafi wa mwisho wa mwezi uliofanyika Mtaa wa Mabibo leo mei 28,2022
Aidha, Beatrice amewapongeza wananchi kwa kushiriki kikamirifu kufanya usafi, na amewaomba kuwa na utamaduni wa kufanya usafi kwenye maeneo ya biashara na majumbani na kuendelea kulipa ada za usafi na kuacha kuwapa wenye matoroli kwani hawatupi dampo na wanaendelea kuchafua mazingira yetu.
Kwa upande wake Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo Jaffary Nyaigesha amewapongeza wananchi kwa kujitokeza kushiriki usafi huo na amewataka kuendeleza utamaduni huo kila siku majumbani mwao na kuacha tabia yakuweka uchafu kwenye mitaro ya maji machafu ili kuendelea kutunza miundombinu hiyo na kufanya mazingira kuwa safi.
Nae Mhe. Joseph Thomas Kleruu Diwani kata ya Mabibo amewasisitiza wananchi kuendelea kusafisha maeneo kila siku na sio kusubiri usafi wa jumamosi na matarajio yake ni kuona kata yake inapata nishani ya usafi.
Wananchi wa kata ya mabibo manispaa ya ubungo wakishiriki zoezi la usafi linafanyika kila jumamosi ya mwisho wa mwezi Mei, 2022
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa