Katika kulinda Afya za wananchi hasa watoto chini ya umri wa mika mitano, miaka miwili na wasichana wizara ya afya kwa kushirikiana na Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo imekuwa ikitoa chanjo mbalimbali kwa makundi hayo ili kuimarisha afya zao na kuwakinga na magonjwa mbalimbali
Hayo yamesemwa leo Januari 27, 2023 na Mganga mkuu wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo katika zoezi la utoaji wa mafunzo kwa watoa huduma kutoka vituo mbalimbali vya afya kuhusu mpango maalumu wa kuimarisha chanjo ya surua kwa watoto chini ya umri wa miaka miwili ambao wamezaliwa kati ya Februari 2020 hadi Aprili 2022. Mafunzo hayo yametolewa na waratibu wa chanjo kutoka TAMISEMI kwa kushirikiana na maafisa wa idara ya Afya Manispaa ya Ubungo katika ukumbi wa Ngome uliopo Sinza Afrikasana
Chanjo hiyo ya surua inatarajiwa kutolewa kwa muda wa siku tano kutoka Februari 01 - 05, 2023 kwa watoto wote ambao hawajapata chanjo ya Surua au hawajakamilisha ratiba ya dozi mbili ya chanjo.Mganga mkuu wa Manispaa ya Ubungo Dokta Peter Nsanya amesema "Uimarishaji wa chanjo ya Surua kwa watoto chini ya miaka miwili ni muhimu sana kwaajili ya kuzuia magonjwa ya mlipuko kwa watoto kama ugonjwa wa Surua" amesema
Chanjo hii kwa Manispaa ya Ubungo inatarajiwa kuwafikia watoto 12,379 na itatolewa katika vituo vyote vya afya vinavyotoa huduma ya chanjo ambapo timu za wahamasishaji watakua wanapita kwenye mitaa yote kuwaelekeza wazazi/walezi wenye watoto chini ya miaka miwili kwenda kwenye vituo hivyo kwaajili ya kuwapatia watoto wao chanjo hiyo
Nae ndugu Given Mlay mratibu wa chanjo kutoka TAMISEMI amewasisitiza watoa huduma ambao wamepatiwa mafunzo hayo kwenda kuifanya kazi hii kwa uadilifu mkubwa ili kuhakikisha malengo ya kutoa chanjo hii yanafikiwa kwa kiwango kikubwa kwa maeneo yote ya Manispaa ya Ubungo
watoa huduma za afya wakipewa mafunzo kuhusu utoaji wa chanjoc
Aidha kwa wazazi/walezi wote wametakiwa kutoa ushirikiano kwenye kufanikisha zoezi hili kwa kuwapeleka watoto wao kwenda kupatiwa chanjo hiyo kwani mtoto ambaye hatopata chanjo hiyo ni hatari kwa afya yake na jamii inayomzunguka. KINGA NI BORA KULIKO TIBA
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa