Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe. Kheri James amewataka Watendaji wa Kata, Mitaa na Wenyeviti wa Serikali za Mitaa wa Wilaya hiyo kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia Maadili, Kanuni, Taratibu na Sheria za Utumishi wa Umma katika kusimamia shughuli mbalimbali za maendeleo katika maeneo yao.
DC Kheri, amewaeleza hayo kwenye kikao kazi kilichofanyika leo Julai 26, 2021 katika ukumbi wa mikutano wa Manispaa hiyo na kueleza kuwa wao kama viongozi wa wajibu wa kusimamia shughuli zote zinazofanyika kwenye maeneo yao Kwa uadilifu na uwajibikaji mkubwa ili kurahisisha utoaji wa huduma kwa wananchi hususani ukusanyaji wa mapato na usimamizi wa miradi ya maendeleo
Shikamaneni kwa kujenga mahusiano mazuri ninyi kwa ninyi na ninyi na wananchi wenu huku mkijiamini na kudhubutu katika utendaji kazi wenu hususani katika kufanya maamuzi kwa lengo la kutekeleza shughuli za Serikali.
"Serikali imewaamini ndio maana imewapa nafasi hizo kuchukueni hatua bila kumwonea mtu ilimradi mnafuata sheria, kanuni na taratibu za Serikali katika kutekeleza kazi za Serikali, Mimi nawaahidi ushirikiano" alisema DC Kheri
Aidha, DC Kheri amewasisitiza watumishi na Viongozi hao kuwa waadilifu hasa kwenye ukusanyaji wa fedha za Serikali kupitia *PoS machine* kwani kumekuwa na changamoto kubwa kwenye eneo hilo.
Upangaji wa malengo yanayoshirikisha wananchi ni kati ya mambo ambayo DC Kheri ameyasisitiza kwa Watendaji na Viongozi hao ikiwa ni njia nzuri ya kujua mambo ya Kutekelezwa Kwa mwaka husika badala ya kufanya kazi Kwa mazoea.
Pamoja na majukumu mengine tambueni tuna janga la ugonjwa wa COVID 19 , fuateni mwongozo wa Serikali wa namna ya kujikinga kwa kunawa mikono Kwa maji tiririka, kuvaa barakoa na kuepuka misongamano isiyo ya lazima kwani ugonjwa upo.
Akiongea kwa niaba ya watumishi hao, Afisa Utumishi na Utawala wa Manispaa hiyo ndugu Selemani Kateti amemshukuru Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya kwa maelekezo mazuri na kuahidi kusimamia utekelezaji wake kwa manufaa ya Manispaa na wananchi wake.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa