Leo Juni 15 mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe. Kheri James ameanza ziara yake ya siku nne ambapo leo ametembelea miradi 6 ili kukagua maendeleo yake.
Mhe. Kheri amekagua miradi ifuatayo;
| Ujenzi wa Shule ya Sekondari ya wasichana Maalumu ya Mkoa - Kwembe
| Ujenzi Kituo cha afya Amani - Kwembe
| Ujenzi shule ya sekondari Msakuzi - Mbezi
| kituo cha Kimara - Saranga
| Ujenzi Kituo cha afya Makuburi
Miradi yote iliyokaguliwa leo, mkuu wa Wilaya ametoa maelekezo ya kuendelea kuboresha kwa kuzingatia ubora na kwa muda uliopangwa kumalizika kabla ya kukabidhiwa rasmi.
Kesho tena Juni 16, ziara ya Mkuu wa Wilaya itakua katika kata ya Goba na Mburahati kuhamasisha zoezi la anwani makazi.
#UbungoYetuFahariYetu
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa