Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe. Kheri James leo Machi 16, 2022 amezindua BODI Mpya ya afya ya wilaya hiyo, na kuitaka bodi hiyo kufanya kazi kwa ufanisi kwa kuhakikisha huduma za afya zinatolewa kwa ubora kwa wananchi.
Akizindua bodi hiyo yenye wajumbe 11, James amewapongeza wajumbe hao kwa kuchaguliwa kusimamia sekta nyeti ya afya ambayo inagusa wananchi na kuwaeleza kuwa kazi kubwa ya bodi hiyo ni kuwakilisha jamii kwa kupokea changamoto zao na kuzitafutia ufumbuzi kwa kushirikiana na uongozi wa Halmashauri.
"Uwepo wenu ni uwakilisha wa umma, toeni ushauri kwa serikali na kuchagiza mabadiliko ya sera ili kuboresha utoaji wa huduma za afya kwa wananchi ambao wamewachagua ili muwe daraja kati ya serikali na wao kwa kupokea changamoto na kuzifanyia kazi" alieleza James
James amesistiza kuwa Bodi ni sauti ya watu wa kawaida hivyo ikasimamie utoaji wa huduma bora kwa uaminifu sambamba na kutatua changamoto katika vituo vya kulolea huduma za afya kwa wakati kabla hazijafika ngazi za juu.
"Mstumie bodi hii kama jukwaa la siasa, fanyeni kazi kwa mujibu wa mwongozo, uadilifu na uwajibikaji wa hali ya juu ili kufikia malengo ya serikali ya kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora wakati wote.
Akiongea na wajumbe hao, Mganga Mkuu wa Manispaa hiyo, Dkt Peter Nsanya ameeleza kuwa, Manispaa ya Ubungo ina jumla ya vituo vya kutolea huduma za afya 162 ambapo kati ya hivyo 22 ni vya Serikali
Aidha, Nsanya ameyataja majukumu mengine ya Bodi kuwa ni kupanga na kupitisha mpango ya bajeti pamoja na kukagua miradi ya maendeleo, kuhakikisha vituo vya afya, hospital, na zahanati vinatekeleza shughuli za Afya, kuhakikisha uwepo wa upatikanaji wa dawa na vifaa.
Uundaji wa Bodi ya Afya upo chini ya Sheria ya Serikali ya Mitaa (Mamlaka ya Wilaya), Sura na 287, Mamlaka ya Miji sura na 288, pamoja na mwongozo wa uundaji na uendeshaji wa Bodi za Afya za Halmashauri na kamati zake wa go mitatu chini ya mwenyekiti wake Ndg Allan Semporo.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa