Aliyosema Mhe. Ng’wilabuzu Ndwata Ludigija Mkuu wa Wilaya ya Ilala akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dar Es salaam Amos Makalla kwenye Maadhimisho ya Mazingira duniani mikoani humo.
•Ikiwa leo ni siku ya Mazingira duniani jiji la Dar Es salaam linaungana na Taifa na dunia Kwa ujumla kuadhimisha siku hii Kwa kauli mbiu isemayo Tumia nishati mbadala kuongoa mfumo wa ikolojia.
•Kutumia nishati mbadala ikiwemo gesi, Umeme na majiko banifu yanayobuniwa na wataalamu mbalimbali ili kuepuka matumizi ya mkaa ambapo Kwa siku moja jumla ya magunia 300,000 hutumika.
•Kupanda miti kwa wingi ili kupendezesha na kutunza mazingira yetu.Niwapongeze TFS kwa jitihada za Kupanda miti kwa wingi.
•Dar ina viwanda, hivyo naagiza wataalamu waendelee kufuatilia viwanda Vinavyotiririsha maji machafu yanayoharimu viumbe vya majini, Wito natoa sheria zitumike kwa wanaojihusisha na utiririshaji wa maji machafu kwenye Makazi ya watu pamoja na kwenye Mito
•Bado uzalishaji, usambazaji na utumishi wa mifuko ya plastic bado upo, natoa wito kwa wana Dar Es salaam kutumia vifungashio vilivyokubalika, Watendaji simamieni Watendaji ipasavyo marufuku ya mifuko ya llastiki
•Katika Mkoa tuna mabonde mengi ikiwemo mto msimbazi wananchi wamekuwa wakitupa taka zinazoathiri viumbe hili nalo sisimamiwe
°Uchimbaji wa mchanga ulenge kusafisha mito na sio vinginevyo wataalamu simamieni ili kutopanua mito inayosababisha madhara kwa wananchi . Uchimbaji uwe kwenye mito iliyochaguliwa
•Mkoa unazalisha takribani tani 450,000 za taka, Niwaagize wakurugenzi kutumia magari ya taka waliogawiwa yanafanye kazi ya kuzoa taka ili Manispaa zetu ziwe Safi
•Usafi unaanzia ngazi za familia kwa kufanya usafi kila mwisho wa mwezi, wafanyabiashara wafanye usafi maeneo yao ya biashara. Serikali itachukua hatua Kwa watu wanaochafua mazingira
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa