Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Kheri James amekabidhiwa ofisi rasmi na aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Ubungo Kisare Makori leo tarehe 28 juni, 2021 katika ukumbi wa mikutano uliopo katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya Luguruni
Akiongea wakati wa makabidhiano hayo Dc Kheri aliahidi kutekeleza yale uliyoaachwa na kuhakikisha mahusiano mazuri Kati ya chama na Serikali na pia ulinzi na usalama wa Wilaya yetu ya Ubungo unaendelea kuimarika
"Nikupongeze nimekuta wilaya iko shwali pia mahusiano mazuri na wadau mbalimbali yako safi na niahidi ntaendeleza Yale yote ambayo ulikuwa umeyafanya kwa kushirikiana na kamati ya ulinzi na usalama, Mkurugenzi ,wakuu wa idara na watalaam" Aliongeza Kheri
Akizungumza baada ya kukabidhiwa ofisi hiyo Kheri amesema kuwa anamshukuru rais wa jamuhuli ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa kututeuwa na nikutakie kazi njema unapokuwa Tabora ( Uyui)
Aidha Kisare alimkabidhi Kheri kitabu cha taarifa na kumshukuru rais wa jamuhuli ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa uteuzi na kuahidi kuendelea kutoa ushirikiano kwa Dc Ubungo
Nae Beatrice Dominic Mkurugenzi Manispaa ya Ubungo amemshukuru Kisare kwa miongozo na malezi bora alipo kuwa Ubungo na kumtakia utekelezaji mwema anapokwenda Tabora(Uyui)
Alikadhalika, Mstahiki Meya Manispaa ya Ubungo Jaffari Nyaigesha amemshukuru DC Uyui kwa ushirikiano mzuri alipokuwa Ubungo na kwa utekelezaji mzuri wa maendeleo ya Wilaya ya Ubungo
Naomba nikukaribishe sana Dc Kheri tuna ahidi kuonyesha ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu yako
Ikumbukwe kuwa aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Kisare Makori ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Uyui Mkoa wa Tabora
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa