Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe. Kheri Denice James ameridhishwa na mikakati iliyowekwa na Manispaa ya U bungo ya kuboresha miundombinu ya shule ikwemo utengenezaji wa madawati na ujenzi wa madarasa katika shule za manispaa hiyo ikiwa ni maandalizi ya kuwapokea wanafunzi wa darasa la kwanza na kitado cha kwanza kwa mwaka 2022.
Mhe. Kheri ametoa kauli hiyo leo juni 23, 2021 wakati wa ziara ya kikazi ya kutembelea miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika manispaa hiyo na kueleza kuwa mkakati wa kujenga madarasa na kutengeneza madawati mapema utaondoa changamoto ya upungufu wa miundombinu hiyo kwenye shule na hivyo kufanya wanafunzi kusoma katika mazingira bora.
“Kwa mwaka 2022 sitegemei Ubungo iwe kati ya Halmashauri zenye changamoto ya upungufu wa madarasa na madawati ikiwa mikakati yetu itatekelezwa kwa ufanisi na hii itafanikwa zaidi jamii na wadau wa maendeleo wakishirikishwa kikamilifu katika kulitekeleza hili, kila mmoja atekeleze wajibu wake” alieleza Mhe. Kheri
Mhe. Kheri ameendelea kusema kuwa, kama idadi ya wanafunzi wanaoratajia kujiunga na kidato cha kwanza kwa mwaka ujao tunayo ni dhahiri mahitaji ya madarasa na madawati yatakayotumika yanajulikana hivyo naagiza madarasa hayo yaanze kujengwa mapema mwezi julai na hadi mwezi disemba yawe yamekamilika tayari kwa kuwapokea wanafunzi januari 2022.
Aidha, Mhe. Kheri amewapongeza wadau wa maendeleo wakiwemo benki ya CRDB, NMB na Kanisa Katoliki kwa mchango wao mkubwa katika kuboresha miundombinu ya shule ya sekondari mashujaa iliyoko kata ya Sinza kwa kujenga madarasa, fensi na utengenezaji wa viti na meza hali inayoifanya shule hiyo kuwa na mazingira mazuri ya kujifunza na kujifunzia
“Huu mkakati wa kuboresha miundombinu katika shule zetu unapaswa kuwa shirikishi ili kila mtu awe na mchango katika kufanikisha zoezi hili mfano mzuri ni katika shule ya sekondari mashujaa ambapo kanisa katoliki limetoa milioni 20 kwa ajili ya ujenzi wa ukuta wa shule, nawashukuru na kuwapongeza sana viongozi wengine tuige mfano wa uongozi wa shule hiinamna ulivyoshirikisha wadau”
Mhe. Kheri amezitaka bodi na kamati za shule zote za Manispaa ya Ubungo kutekeleza majukumu yao ipasavyo katika kusimamia na kubuni mikakati itakayozifanya shule zetu kuondokana na changamoto mbalimbali ikiwemo madarasa na madawati badala ya kusubiri serikali pekee itatue changamoto hizo.
“ifike wakati bodi na kamti za shule zishindanishwe kwa ubunifu wa kuboresha miundombinu ya shule hii itasaidia kuwakumbusha wajumbe majukumu yao ya msingi badala ya kufanya kazi kwa mazoea” alielekeza Mhe. Kheri.
Akieleza moja ya mkakati wa manispaa, Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Beatrice Dominic amesema kuwa pamoja na ujenzi wa madarasa unaoendelea katika shule mbalimbali, kwa mwaka mpya wa fedha unaonza mwezi Julai 2021 manispaa imepanga kujenga madarasa 100 lengo likiwa ni kuhakikisha changamoto ya upungufu wa madarasa na madawati inapungua kwa kiasi kikubwa.
Mhe. Mkuu wa Wilaya Ubungo ametembelea miradi yenye thamani ya shilingi bilioni 59.8 ikiwemo mradi wa ujenzi wa kituo kikuu cha mabasi cha magufuli kilichogharimu bilioni 56.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa