Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe. Kheri James ametatua mgogoro wa ardhi eneo la Bwawa Mtaa wa Temboni kwa kusitisha ujenzi unaofanyika katika eneo hilo na anayesadikika kuwa mmliki wa eneo hilo na kusema eneo hilo litakuwa mali ya Umma kwa sasa.
Mhe. Kheri amefikia uamuzi huo baada ya wananchi wa mtaa huo kutoa malalamiko kuwa wanapata shida ya nyumba zao kujaa maji kipindi cha mvua kutokana na mwekezaji huyo kuweka kifusi sehemu ya njia ya maji pamoja na kujenga kalvati dogo ambalo halipitishi maji vizuri.
Maamuzi hayo ameyatoa Julai 27, 2021 kwenye kikao kilichohusisha wananchi wa eneo hilo pamoja na viongozi wa serikali ngazi ya Mtaa, Kata na Halmashauri, ambapo Mhe. Kheri amesema, kutokana na sheria ya ardhi eneo la Bwawa halimilikiwi na mtu binafsi kwa sababu haliwezi kufanyia maendelezo yoyote, hivyo ni mali ya Umma.
Aidha,Mhe.kheri ameagiza kuwa kifusi kilichowekwa kwenye eneo hilo kinacho sababisha hofu ya kutuamisha maji kipindi cha mvua nakuathiri wananchi kitolewe haraka ili wananchi wasipate madhara wanayiyapata sasa ikiwemo vyoo kujaa haraka.
"Nategemea baada ya maamuzi haya Mtaa wa Temboni utakuwa tulivu na kazi ya serikali ni kuhakikisha kero za wananchi zinatatuliwa"alieleza Mhe.Kheri.
Pia , Mhe. Kheri ameamuru kifusi kinachoonekana kuleta hofu kwa watu kiondolewe ili maji yaendelee kupita.
Wakazi wa mtaa wa temboni wameridhika na maamuzi ya utatuzi wa mgogoro huo nawapo tayari kushirikiana na wataalamu katika utekelezaji wa maagizo yaliyotolewa katika mgogoro huo.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa