Yatakiwa kukamilisha kazi hiyo mapema
Wananchi wamechangia Jumla ya shilingi bilioni 9.4 kwa ajili ya upimaji
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mheshimiwa Kheri James amekutana na Makampuni ya Upangaji na Upimaji ardhi katika Wilaya hiyo ili kujadili changamoto zinazoyakabili makampuni hayo na kutoa maelekezo ya kukamilisha zoezi hilo kwa wakati ili wananchi waweze kumilikishwa maeneo yao.
Mkuu wa Wilaya ameamua kufanya kikao hicho kutokana na wananchi wengi wa Wilaya hiyo kutoridhishwa na mwenendo wa utendaji kazi wa makampuni hayo licha ya kuchukua *fedha kwa wananchi shilingi bilioni 9.4 kwa ajili ya kugharamia upimaji
Kutokana na hali hiyo, Mhe.Kheri ameyasisitiza makampuni hayo kufanya kazi kwa haraka na weledi huku wakizingatia mikataba ya kazi yao ili mchakato wa utoaji hati ufanyike na wananchi wamilikishwe maeneo yao kwa mujibu wa sheria
"Kama Serikali ilivyowaamini na kuwapa kazi basi tunzeni hedhima hiyo Kwa kuhakikisha mnakamilisha mchakato wa urasimishaji ili Wananchi wapate hati miliki za maeneo yao" Mhe. Kheri
Akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa miradi ya urasimishaji katika Wilaya, Afisa Ardhi wa Manispaa ya Ubungo Fadhili Hussein ameeleza kuwa wilaya *ina Jumla ya makampuni 19 ya upangaji na 18 ya upimaji yanayotekeleza kazi za urasimishaji katika Mitaa 60 ndani ya kata 11
Aidha, ameendelea kueleza kuwa Jumla ya viwanja *176,350* vilianishwa huku viwanja vilivyopimwa na kuidhinishwa ni 17,776
Sawa na asilimia 10 tu ambapo wananchi wamechangia shilingi mbilioni 9.4 Kwa ajili ya zoezi hilo.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa