Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Mhe. Kheri James ametoa siku saba kwa wazabuni wa uwekaji wa vibao vya anwani za makazi pamoja na watendaji wa kata na mitaa ndani ya wilaya ya Ubungo, kuhakikisha wanakamilisha zoezi hilo.
Mhe. James ametoa agizo hilo leo Juni 16, 2022 wakati akiendelea na ziara yake ambapo leo ilikua ni zamu ya kata ya Goba na Mburahati kwenye ukaguzi wa zoezi la anwani za makazi na kuhamasisha ushiriki wa zoezi la Sensa kwa wananchi na wakazi wa Kisiwani, Mburahati kufuatia kata hiyo kuwa ni miongozi mwa kata ambayo haikufanya vizuri katika zoezi la anwani za makazi huku kwa wilaya nzima ya Ubungo, zoezi likiwa limefikia asilimia 57 ambapo tayari nyumba zote zina namba na zoezi linaloendelea ni la kuweka vibao vya namba kwa nyumba zote zilizosalia.
Kwa upande wake Diwani kata ya Mburahati, Mhe. Yusuph Omari Yenga amesema watahakikisha zoezi hilo linaendelea vizuri katika kata hiyo huku akiahidi kutekeleza maagizo yote yaliyotolewa na Mkuu wa Wilaya ya kwamba ndani ya siku saba zoezi hilo liwe limekamilika.
#kaziiendelee #UbungoYetuFahariYetu
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa