Mapema leo Februari 18, 2023 Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe. Hashim Komba amefanya ziara katika eneo la Mbezi Luis kuona barabara yenye changamoto kubwa ya ubovu ambayo ina urefu wa kilomita tatu inayoanzia kwa Robert mpaka Kavimbirwa
Ziara hiyo imefanyika kufuatia wananchi wanaoishi eneo hilo kuanza taratibu za kutatua changamoto hiyo kwa kufanya michango mbalimbali ya fedha na vifaa ili kurekebisha maeneo yote korofi ya barabara hiyo.
Akiongea katika ziara hiyo katibu wa kamati ya wananchi ndugu Eddy Eneza amesema kuwa wao kama wananchi wa eneo hilo waliamua kuchangishana fedha ambapo Januari 29, 2023 wananchi hao walikaa kikao na kuidhinisha bajeti ya shilingi Milioni 11,675,000 kwaajili ya ukarabati wa maeneo korofi ambapo mpaka sasa wameshakusanya jumla ya kiasi cha shilingi Milioni 6,465,000 na ahadi za jumla ya shilingi Milioni 7,430,000. kwaajili ya kuanza rasmi hatua za ukarabati wa barabara hiyo. Leo pia kwenye ziara hiyo imepokelewa ahadi ya shilingi Milioni 2,000,000 kutoka kwa Mbunge wa Kibamba Mhe. Issa Mtemvu
Nae Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe. Hashim Komba wakati akizungumza na wananchi hao, amewapongeza kwa kushiriki kwenye mipango ya maendeleo na amewahakikishia kuwa mpango wao kurekebisha maeneo yote korofi ya barabara hiyo yanakamilika kwa asilimia mia moja bila kuwa na kikwazo chochote
"Miundombinu ya barabara katika taifa lolote ni sawasawa na mishipa ya damu kwenye mwili wa binadamu inavyofanya kazi, hivyo barabara ni muhimu sana kwa uchumi wa nchi yoyote ile na sisi ubungo tutahakikisha miundombinu korofi yote ya barabara inatatuliwa" alisema Mhe. Komba
Vilevile Mhe. Komba ameiagiza Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo kutoa greda na compact (Shindilia) kwaajili ya kuchonga na kurekebisha barabara hiyo. Pia Mhe. Komba ameiagiza TARURA kutoa utaalamu wao kwenye ukarabati wa barabara hiyo ili itakapofika Mwisho wa mwaka huu wa fedha Juni 30, 2023 barabara hiyo iwe imekamilika tayari
Nae mzee Bhalijuye fred ambaye ni mwananchi wa Mbezi Luis amemshukuru sana Mhe.Komba kwa kufika eneo hilo na wao wapo tayari kumpa ushirikiano kwenye shughuli mbalimbali
ReplyForward |
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa