Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe. Hashim Komba amewataka watumishi wa Wilaya hiyo kusimamia ukusanyaji wa mapato, utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo na kutatua kero za wananchi.
Matakwa hayo ameyasema katika kikao kazi kilichofanyika leo tarehe 07/02/2023 kilichojumuisha wakuu wa idara na vitengo, Watendaji wa Kata na Mitaa kwa lengo la kujadili utendaji kazi na kuweka mikakati ya pamoja juu ya kuwatumikia wananchi ipaswavyo.
Mhe. Komba ameendelea kusema kuwa ataendelea kuwatumikia wananchi kwa kuhakikisha wanapata huduma bora kama ambavyo alivyoaminiwa na Rais wa awamu ya sita kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu huku akisimamia kauli ya neno MKUU
Lenye maana ya;
M- Mapato
K- Kusikiliza kero za wananchi
U- Usimamiaji wa miradi ya maendeleo
U- Ulinzi na usalama na
U- Usafi wa mazingira
Na alisisitiza kuwa MKUU ndio vipaumbele vyake.
“Kila Mtendaji wa Kata anajukumu la kukusanya mapato sambamba na kuvielewa na kuvisimamia vyanzo vyote vinavyopatikana kwenye maeneo yenu” Alisisitiza Komba.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Ndg. Beatrice Dominic ameendelea kusisitiza watendaji hao kuendelea kuwa wazalendo katika usimamizi na ukusanyaji wa mapato na kuwataka kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia sheria kanuni na taratibu na kuacha kufanya kazi kwa mazoea.
Akiongea Ndg. Iddi Mnyeke kwa niaba ya watendaji wote ameahidi kwenda kuyafanyia kazi maelekezo yote yaliyotolewa ikiwa ni pamoja na kusimamia ukusanyaji wa mapato, kusikiliza na kutatua kero za wananchi, kusimamia miradi mbalimbali ya maendeleo na kuendelea kuwajibika kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa