Kufuatia mabadiliko ya wakuu wa Wilaya ambao yalifanywa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan Januari 25, 2023, leo Januari 31, 2023 Mkuu mpya wa Wilaya ya Ubungo Mhe. Hashim Komba amefika katika ofisi ya Wilaya ya Ubungo kwaajili ya makabidhiano ya ofisi na mkuu wa Wilaya aliyepita Mhe. Kheri James ambaye kwa sasa amehamishiwa wilaya ya Mbulu mkoani Manyara
Hafla hiyo ya Makabidhiano imefanyika katika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa Wilaya ya Ubungo ambapo ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Wilaya na Manispaa ya Ubungo, viongozi wa chama cha Mapinduzi CCM pamoja na wadau wa maendeleo benki ya NMB
Wakati anaongea mkuu wa wilaya ya Mbulu Mhe. Kheri James amechukua fursa hiyo kuwashukuru watumishi wa wilaya na manispaa ya Ubungo, viongozi wa Chama Cha Mapinduzi, Watumishi wa Umma pamoja na wananchi wote wa wilaya ya Ubungo kwa ushirikiano mkubwa ambao walimpatia kipindi cha utumishi wake katika Wilaya ya Ubungo.
Aidha Mhe. James amewaomba watumishi na wananchi wa Ubungo kuendelea kumpa ushirikiano mkubwa Mhe. Hashim Komba ili kumpa nguvu zaidi katika utumishi wake wa kuwatumikia wananchi
m
Makabidhiano ya ofisi kati ya aliyekuwa DC ubungo Mhe.kheri james na Mkuu wa wilaya mpya wa ubungo Mhe.Hashim Komba
Nae Mkuu mpya wa Wilaya ya Ubungo Mhe. Hashim Komba pamoja na kuwashukuru watumishi kwa mapokezi mazuri lakini pia ameainisha vipaumbele vyake katika uongozi wake ikiwa ni pamoja na kuendeleza mazuri yote yaliyofanywa na mtangulizi wake Mhe. Kheri James, kuhakikisha Ubungo inakuwa kinara kwenye kila jambo linalohusu maendeleo, kushughulikia kero za watumishi wa umma pamoja na wananchi wa Wilaya ya Ubungo
Mhe. Komba amesema "Wilaya ya Ubungo ni wilaya changa lakini yenye kasi kubwa ya maendeleo. Mimi kama mkuu wenu mpya wa Wilaya ninaahidi kutoa ushirikiano wangu mkubwa ili kuhakikisha Ubungo inakua ya kwanza kwenye shughuli mbalimbali za Maendeleo" Alisema
Vile vile Mhe. Hashim Komba amemshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kumuamini kwenye kumsaidia majukumu ya kuiongoza Wilaya ya Ubungo.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa