Mkuu wa Wilaya ya Ubungo mhe Kisare Makori ameiagiza Manispaa ya Ubungo kuongeza kasi ya umaliziaji wa jengo la utawala la Manispaa hiyo ili kurahisha utoaji huduma kwa wananchi pamoja na kuwa na mazingira mazuri ya kufanyia kazi kwa watumishi wa Manispaa hiyo.
Mhe. Makori ametoa agizo hilo leo tarehe 30 desemba, 2020 wakati alipotembelea na kukagua utekelezaji wa mradi huo akiwa ameongozana na kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya hiyo na kueleza kwamba Serikali ya awamu ya tano inahitaji miradi itekelezwe kwa wakati na kwa kuzingatia viwango lengo ikiwa nikurahisisha utoaji huduma kwa wananchi.
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo mhe. Kisare Makori (mwenye t-shirt ya mistari) akiwa na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama wa wilaya hiyo pamoja na wataalamu wa Manispaa ya Ubungo wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya kukagua utekelezaji wa jengo la Ofisi za Utawala Manispaa ya Ubungo leo tarehe 30.12.2020
"Baada ya kuvunja mkataba na TBA kutokana na ucheleweshaji wa mradi, Manispaa imewapa kazi nyinyi local fundi ili mradi uishe kwa wakati lakini utekelezaji wenu bado unasuasua, naagiza kufikia tarehe 7 januari 2021 kila fundi awe amemaliza kazi aliyopewa kwa mujibu wa mkataba wake "alieleza Mhe Makori
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo, Beatrice Dominic alisema kuwa Manispaa itajitahidi kuwasimamia mafundi kufanya kazi usiku na mchana ili kufikia januari 2021 kazi zote ambazo zinafanywa kwa sasa ziwe zimekamilika na jengo kutumiwa katika hali ya utulivu.
Beatrice ameeleza kuwa kwa sasa kazi zinazofanyika ni uwekaji wa Umeme, mifumo ya maji taka, ufungaji wa milango na upakaji rangi. Kazi zote mafundi wapo wanafanya kazi na fedha zipo " tutajitahidi kuwasimamia wafanye kazi kwa muda tuliokubaliana"
Ili kuhakikisha kazi zote zinafanyika kwa usahihi na ubora unaotakiwa, Beatrice alieleza kuwa Manispaa ya Ubungo imetafuta wataalamu mshauri kwenye masuala ya umeme na uwekaji wa mifumo ya TEHAMA ambaye atashirikiana na mafundi kuhakikisha kazi hizo zinafanyika kwa viwango vinavyotakiwa.
Mradi huo unajengwa kwa gharama ya shilingi bilioni 6.2 ambapo kati ya fedha hizo bilioni 1.9 kutoka mapato ya ndani na zaidi ya bilioni 4 ni fedha kutoka serikali Kuu.
Jengo la Utawala la Manispaaya Ubungo likiwa kwenye hatua za umaliziaji.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa