Mkuu wa Wilaya ya Ubungo jijini Dar Es salaam Mhe Kisare Makori anatarajia kupokea msaada wa fedha shilingi milioni 230 kutoka kampuni ya Yapi Merkezi kwa ajili ya kujenga miundombinu ya Shule za Msingi na Sekondari wilayani humo.
Kampuni ya Yapi Merkezi inayofanya kazi ya ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) imetoa ahadi hiyo Leo januari 26, 2021 kwenye kikao kilichofanyika kwenye Ofisi ya Mkuu wa Wilaya hiyo na kueleza kuwa msaada huo ni sehemu ya wajibu wa kampuni kusaidia jamii katika changamoto mbalimbali.
Akiongea baada ya kupokea ahadi hiyo, Mkuu wa Wilaya huyo, ameishukuru kampuni hiyo kwa msaada wao katika kuboresha miundombinu ya Shule hususani Madarasa na madawati ambayo kwa sasa uhitaji wake ni mkubwa.
"Kwa niaba ya Serikali na wananchi wa Wilaya ya Ubungo napenda kuishukuru kampuni ya Hapi Merkezi kwa msaada wao kwani utasaidia kupunguza changamoto ya upungufu wa madarasa, madawati na vyoo kwenye shule zetu" ameeleza Makori
Mkori ameendelea kueleza kuwa , msaada huo utaelekezwa kwenye shule zenye changamoto kubwa zaidi ya madarasa na madawati ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa agizo la Serikali la kuhakikisha wanafunzi wote hawakai chini wala kusomea nje.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo, Beatrice Dominic ameeleza kuwa ujenzi wa vyumba 37 kwa ajili ya kidato cha Kwanza unaendelea na madawati 2000 yameagizwa na yameanza kupokekelewa na kusambazwa kwenye shule zenye upungufu.
Aidha Beatrice amewaomba wadau wengine kuendelea kuchangia sekta ya elimu kwani uhitaji wa miundombinu ya Madarasa, madawati na vyoo kwa ajili ya kuboresha mazingira ya kujifunza na kujifunzia bado ni mkubwa sana.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Beatrice Dominic akitoa maelezo ya hali ya miundombinu kwa wawakilishi kutoka kampuni ya Yapi merkezi wakati walipotembelea shule ya msindi Bwawani leo tarehe 26 januari, 2021
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa