Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mheshimiwa Kheri James mapema leo tarehe 23 Mei 2022 amemwakilisha Mkuu wa Mkoa katika ufunguzi wa Kongamano la Kimataifa la ukusanyaji na uchakataji wa taka ngumu lililofanyika katika ukumbi wa chuo kikuu Cha Dar Es Salaam
Akifungua kongamano hilo amewashukuru wadau,sekta binafsi,Serikali katika kuboresha usafi wa majiji na kubuni fursa za kuongeza thamani ya taka ngumu zinazozalishwa Kila siku
Aidha amesema kuwa inakadiliwa jiji la Dar Es Salaam linazalisha taka zaidi ya tani 5,600 kwa siku na uzalishaji wa taka ngumu unakua kwa asilimia 50-60
Aliendelea kwa kusema kuwa, Nimefurahi kuona Taasisi na Mashiriika na vikundi mbalimbali vinaunga mkono juhudi za Serikali katika kuboresha mazingira na maisha ya wananchi hasa wa kipato Cha chini
"Viwanda vya kuchakata taka hutengeneza ajira kwa vijana na Wakina mama na kulifanya jiji letu kuwa Safi" Aliendelea kueleza kheri
Alikadhalika, Makamu Mkuu wa chuo kikuu Cha Dar es salaam Proffesa William Anangisye ameendelea kuwashukuru waandaaji wa kongamano hilo ambalo limekutanisha wadau mbalimbali , Maafisa wa Serikali na viongozi ambalo linalenga kuleta mazingira bora katika swala zima la uchakataji wa taka ngumu ambao unaenda kuleta masilahi makubwa ikiwemo ajira na kufungua fursa mbalimbali
|
|
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa