Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe. Kherry Dennis James ameahidi kuchapa kazi na kuleta nafuu kwa wananchi wa Ubungo kwa kusimamia ulinzi na usalama, usafi wa mazingira na kusikiliza kero za wananchi kama ilivyoelekezwa na Mkuu wa Mkoa huo wa Dar es Salaam
Hayo ameyasema leo juni 21, 2021 kwenye hafla ya kuapishwa kwa wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Dar es Salaam iliyofanyika katika ukumbi wa Anatroglo uliopo Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
"Namshukuru Mungu kwa fursa hii ya kuaminiwa na Rais wa Jamuhuli ya Muungano wa Tanzania kwa kuniamini Mimi na wenzangu kuwatumikia wananchi kwa dhamani hii na ahidi kuwa mtumishi wao na sio mtawala" alisema hayo Dc Ubungo
Aidha akiongea baada ya kuwaapisha wakuu wa Wilaya hao Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Amos Makalla amewataka kutekeleza majukumu kwenye maeneo yao kwa uweledi na ufanisi ili kufikia malengo na kutatua kero za wananchi
Wakuu wa Wilaya hao wameelekezwa kusimamia ukusanyaji wa mapato, usafi wa mazingira, usimamizi wa miradi wa maendeleo, utatuzi wa kero za wananchi pamoja na kusimamia ulinzi na usalama katika maeneo yao
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa